Monday, 21 May 2018

Haji Manara Afunguka Kuhusu Picha Zake Zinazosambaa


Baada ya kusambaa kwa video na picha zinazomwonesha msemaji wa Simba Haji Manara, akihuzunika uwanjani huku akiwa ameshika eneo la moyo amemtaja (Ankal Michuzi) ambaye ni mpiga picha wa Ikulu na alimruhusu kuzisambaza.

Manara ameeleza kuwa lengo la kuzisambaza video hizo ni kuwaonesha mashabiki nguvu ya mchezo wa soka ilivyo kubwa na wao kama viongozi huwa wanaumia pia pindi mambo yanapokuwa hayaendi vizuri.

''Anko Michuzi (mpiga picha wa Ikulu) ndiye ambae alipiga picha na video zote 'zinazotrend' mitandaoni bila mm kujijua, aliniuliza kabla ya kuziachia nikamruhusu ili Watanzania waone tunavyopagawa na hizi timu'', amesema.

Picha na Video hizo zilipigwa kwenye uwanja wa taifa juzi kwenye mchezo wa ligi kuu ambao ulikuwa maalum kwa Simba kukabidhiwa ubingwa lakini furaha yao ilitibuliwa na Kagera Sugar kwa kufungwa bao 1-0. Okwi alikosa penati ambayo ilidakwa na Juma Kaseja.

Ubingwa wa ligi kuu msimu huu ni wa kwanza kwa Simba tangu Haji Manara awe msemaji wa timu hiyo, na amekuwa akiusubiri kwa hamu huku akiwa ni miongoni mwa wanasimba ambao waliokuwa wanajivunia rekodi ya kutopoteza mchezo msimu huu.

No comments:

Post a comment