Tuesday, 29 May 2018

DR Congo yatoa tahadhari kwa taifa lolote litakalotaka kuyumbisha usalama wa taifa

Lambert Mende , msemaji wa serikali JK Kongo atahadharişsha yeyote yule atakaejaribu kuyumbisha usalama wa taifa.

Hayo yamefahamishwa kufuatia  mataimshi ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Jumatano kuwa   anaunga mkono pendekezo la Umoja wa Afrika kwa ushirikiano na Angola kuhusu Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekemea  Jumatatu na kutahadharisha  taifa lolote ambalo litaingilia kati uhuru wa JK Kongo  kwa ushirikiano na mataifa ya Magharibi.

Kwa mujibu wa Lambert Mende, msemaji wa serikali ya Jk Kongo ni njama iliowazi dhidi ya  taifa huru. Hayo Lambert Mende ameyazungumza hayo kufuatia  matamshi ya rais wa Ufaransa kwa waandishi wa habari  akiwa na rais Paul Kagame kuwa ana unga mkono Umoja wa Afrika kwa ushirikiano na  rais wa Angola kuhusu JK Kongo.

No comments:

Post a Comment