Sunday, 20 May 2018

Bonge la Nyau Avilaumu Vyombo vya Habari Kuhusu Q Chief

Msanii wa Bongo Flava, Bonge la Nyau ametupa lawama kwa vyombo vya habari kwa kile alichodai vinapendelea baadhi ya wasanii na kuacha wale wenye vipaji vya kweli kama Q Chief.

Muimbaji huyo amesema vyombo vya habari vimekuwa vikiangalia maslai binafsi zaidi kuliko muziki wa msanii kitu ambacho kimekuwa kikiwaumiza wasanii wengi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika mengi, hayo ni baadhi;

"Kiukweli kuna baadhi ya watu wameaminiwa na media kubwa na kupewa nafasi za kupush muziki wetu ili uwafikie jamii ila wao ndio wamekuwa waharibifu wakubwa wa huu muziki kwa kujenga matabaka na kuwagawa watu

"Leo hii akitoa kazi huwezi kuiskia ikipewa nafasi kubwa kwenye radio wala tv station kama baadhi ya wasanii wanavyopewa hiyo air time, ukiulizwa utaambia Ohoo wakati wake umeisha, mara alikuwa mjeuri kipindi yupo juu.

"Wengine watakwambia madawa yamemchanganya but ukiskiza kazi zake mpya ina ubora kuliko hata hao wanaowaona wa maana kwa kipiki hicho.Wadau wamekuwa wakiangalia sana biashara zao kulizo talent au kazi nzuri inayowafikia, leo hii nyimbo haiwezi kutoka from no where na kufanya vizuri nchi nzima kama ilivyokuwa ikitokea miaka ya nyuma.

"Cha kushangaza kingine chart ya mziki kwenye kituo A ni tofauti kabisa na kituo B na C, hii inatugawa sana na inasababisha nyimbo nyingi zisiwe kubwa atuwezi kufika kwa style hii, watu kuangalia maslai yao binafsi na kujuana.

"Media nyinyi ndo kila kitu kwenye huu muziki wetu bila ya nyinyi hakuna sisi, hata mtu anapotokea kuteleza na kutofautiana nae yawapasa kumwangalia tena kwa jicho la pili, Q chief anahitaji huruma yenu pia, ni kipaji na msipoangalia ataangamia halafu tuanze kutafutana uchawi.

May 14, 2018 kulianza kuenea kwa taarifa kuwa Q Chief ameacha muziki na alipotafutwa alieleza mengi ambayo anayapitia katika maisha yake kwa sana pamoja na dhamira yake ya kutaka kuacha muziki.

No comments:

Post a comment