Saturday, 12 May 2018

Bodaboda Lindi waliangukia jeshi la polisi

Na.Ahmad Mmow
LICHA yakuhaidi kutii sheria bila shuruti,wasafirishaji wa abiria kwa pikipiki na bajaji (bodaboda)katika manispaa ya Lindi.Wameliomba jeshi la polisi mkoani humu kutumia njia zitakazo wapa uhakika wakuwa salama wao wenyewe na vyombo vyao vya usafiri pindi wanapokamatwa na jeshi hilo.

Wito huo ulitolewa jana wakati wa mkutano wa wasafirishaji hao uliofanyika katika uwanja wa mchezo wa mpira wa miguu wa Ilulu uliopo katika manispaa ya Lindi.Ambao ulihudhuriwa pia nakamanda wa kikosi cha usalama barabarani wa mkoa wa Lindi.

Walisema hawapingi jeshi hilo kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria,naliendelee kuwakamata wanaovunja sheria za usalama barabarani.Hata hivyo waliomba njia zinazotumiwa kuwakamata zisisababishe wahalifu kurahisishiwa kazi ya kuwaibia vyombo vyao vya usafiri na kuhatarisha usalama wao.

Abasi Muwachi wakituo cha soko kuu alisema kitendo cha askari wa jeshi hilo kuwakamata usiku wakati hawajavaa sare kinaweza kutumiwa vibaya na wezi ambao wanaweza kujifanya ni askari wa jeshi hilo nakujipatia pikipiki kiulaini bila kubughuziwa.

Alisema kwakuwa askari hawavai sare nirahisi hata wezi kuaminiwa na kukabidhiwa vyombo vyao.Hata hivyo watakapofuatilia kituoni watakataliwa nakuambiwa waliowapa vyombo vyao usiku hawakuwa askari wa jeshi hilo,bali wezi.

"Sisi tutajuaje kama hawa niaskari au niwezi.Mtindo huu ukizoeleka nilazima tutaibiwa.Kwasababu wote tutajua kwamba askari hawavai sare,tutawakabidhi wezi vyombo vyetu bila kujua .Lakini asubuhi tutakapokuja kituoni ndipo tutakapojua kwamba tumeibiwa," alisema Abasi.

Mwendesha pikipiki huyo aliongeza kusema kwamba licha ya hofu ya kuibiwa,lakini pia njia hiyo itasababisha uvunjifu wa mahusiano mema baina askari wa jeshi hilo nawaendesha bodaboda hao.Kwamadai kwamba nivigumu wao kukabidhi  pikipiki na bajaji zao kwa watu wasiowajua.Hivyo watalazimika kupambana nao bila kujua kwamba wanaopambana nao ni askari.Kwasababu hawana tofauti na raia wakawaida.

Mwendesha bodaboda mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Kibuga Rostasi  alisema kitendo cha askari kutovaa sare,tena nyakati za usiku kinaweza kutafsiriwa vibaya.Kwamba kinachofanywa na askari hao hakipo kisheria na hawajaagizwa.Bali wanafanya kwa utashi wao kwaajili ya masilahi yao binafsi.

Nae Mjinja Sabi licha ya kuunga mkono maelezo ya wenzake alitoa wito kwa jeshi hilo kutoa ushirikiano na waendesha bodaboda.Ikiwamo kutumia lugha za kistaharabu badala ya vitisho na dharau.Kwani kwakufanya hivyo wataogopwa na kukosa ushirikiano ambao ni muhimu katika kufanikisha utendaji na majukumu yao.

"Hatuwezi kulaumu kutufikisha mahakamani na hatuwazuii kutimiza na kutekeleza wajibu wenu.Tena nibora kupelekwa mahakamani kuliko kutupiga fimbo au vibao usiku,mkikosa ushirikiano nasisi mtafanya kazi kwa ugumu sana," alisema Sabi.

Akijibu malalamiko na maombi ya waendesha bodaboda hao,kamanda wakikosi cha usalama barabarani wa mkoa wa Lindi,mrakibu msaidizi mwandamizi wa polisi(SSP),Abdi Issango alisema wamelazimika kubadili mbinu za kuwakamata wanaovunja sheria baada ya waendesha bodaboda kutoheshimu sheria.Ikiwamo kukataa kusimama wanaposimamishwa baada ya kubaini wanasimamishwa na askari wa jeshi hilo.

Alisema jeshi la polisi linatambua umuhimu wa waendesha Pikipiki na biashara wanayofanya.Kwahiyo halina chuki nao.Bali wanalazimika kubadili mbinu kila itakapohitajika pindi wahalifu watakapo endelea kubadili mbinu katika kutekeleza vitendo vya kihalifu.

"Mimi nalipwa mshahara kwa kazi ya kusimamia sheria halali zisivunjwe,kwahiyo niwajibu wangu kuhakikisha sheria hazivunjwi.Hatunashida kabisa na mtu anaetii sheria.Mimi nikiongozi katili kwa wasio tii sheria,lakini nirafiki wa wanaotii sheria bila shuruti,"alisema Issango.

Kamanda huyo alibainisha kwamba jeshi hilo lipo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi bila chuki.Huku akitoa wito kupelekewa taarifa za askari wanatenda kazi zao kinyume cha taratibu,kanuni na sheria za jeshi hilo.Bali wao(waendesha bodaboda) wasiwe chanzo cha kulifanya jeshi hilo kubadili mbinu za kukabiliana nao kutokana nakuendelea kuvunja sheria siku hadi siku.Tena kwambinu tofautitofauti.

Kwaupande wake ofisa mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti wa vyombo vya majini na nchi kavu(SUMATRA) mkoani humu,Andrew Mlacha alitoa wito kwa wasafirishaji hao kusoma masharti na maelekezo yaliyomo kwenye leseni zao.Huku akitoa wito kwa wasio naleseni wakakate ili kuepuka usumbufu usio nasababu

No comments:

Post a comment