Friday, 18 May 2018

Baada ya Alikiba kuzindua MoFaya, Nandy naye Azindua Sabuni na Mafuta Yake

Ikiwa ni wiki mbili zimepita tangu msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba kuzindua kinywaji  chake cha Mofaya, hatimaye msanii mwingine wa muziki, Mrembo Nandy naye amejitupa kwenye ujasiriamali.

Nandy amesema kuwa ameingia ubia na kampuni ya Grace Products inayojihusisha na utengenezaji wa sabuni za kuogea na vipodozi mbali mbali vya asili na yeye atakuwa ni moja ya wamiliki wa kampuni hiyo.

Akifunguka kuhusu dili hilo jana Mei 17, 2018 mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam, Nandy alisema bidhaa zote za vipodozi na sabuni vitakuwa na jina na picha zake na kuwataka mashabiki wake wamuunge mkono kwa kununua bidhaa zake.

No comments:

Post a comment