Tuesday, 29 May 2018

Alikiba ampa shavu Mpoki

Katika kuelekea mchezo maalumu wa hisani ya kuchangia elimu, msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba ametangaza kikosi cha wachezaji watakao kuwa upande wake kupambana dhidi ya  kikosi cha wachezaji watakaokuwa upande wa mshambuliaji wa timu ya Taifa na klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta.
Picha inayohusiana
Alikiba
Kwenye kikosi hicho, Alikiba amemchukua mshambuliaji hatari wa klabu ya Simba, Emmanuel Okwi na wachezaji wengine kama John Bocco, Msuva, Erasto Nyoni, Abdu Kiba na wengineo kama inavyoonesha hapa chini kwenye picha.
Kikubwa zaidi ni kwamba Alikiba amemchagua mchekeshaji maarufu nchini Tanania, Mpoki kuwa msemaji wa timu yake aliyoichagua.

No comments:

Post a comment