Saturday, 21 April 2018

Zari amlilia Masogange, ‘kila mwezi alinitumia sms’

Bado wasanii na watu mbali mbali wenye ukaribu na tasni ya burudani Bongo wanatoa salamu za pole kufuatia kifo cha video vixen, Agness Gerald ‘Masogange’, Zari The Boss Lady naye hajakaa kimya.

Zari ameeleza kuwa Masogange alikuwa akimtafuta kupitia simu kila mwezi akimuulizia maendeleo ya watoto wake ingawa hawakuwa marafiki sana. Kupitia mtandao wa Snapchat Zari ameandika;
We were not friends as such but ever since you got my number you’ve been dropping me a text every month and i mean no month passed without you asking how are the kids. in peace sis.
Masogange enzi za uhai wake aliweza kutokea kwenye video za wasanii kama AY na Mwana FA, Belle 9, Tunda Man, Izzo Bizness na wengineo. Amefariki jana April 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar es Salaam.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: