Wednesday, 11 April 2018

Yanga yashindwa kutamba mbele ya Singida United


Ligi kuu soka Tanzania Bara imeendelea tena hii leo kwa michezo kadhaa kupigwa kwenye viwanja mbalimbali huku bingwa mtetezi klabu ya Yanga SC ikilazimishwa sare ya bao 1 – 1 dhidi ya Singida United uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Bao la Singida United likifungwa na Papy Kambale dakika ya pili ya mchezo huo wakati Yanga SC ikisawazisha kupitia kwa Abdalla Shaibu kunako dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza.

Yanga SC na Singi United hazijawahi kufungana ndani ya dakika 90 toka kukutana kwao wakati kwenye michezo mingine dimba la Mwadui Complex mjini Shinyanga. Mwadui FC 2-1 Lipuli FC, Mbao FC 2 – 1 Njombe Mji, Standa United 1 – 3 Maji Maji,

Simba SC kesho itashuka dimbani kuikabili Mbeya City wakati Yanga SC wakisafiri kwenda kucheza mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi Welayta Dicha.

No comments:

Post a comment