Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewataka wanawake waliotelekezwa na wabunge wafike kwake au wamuandikie barua huku wakiwa na DNA Certificate.
Spika Ndugai ameyasema hayo, Bungeni mjini Dodoma kabla ya kuhairisha kikao cha sita cha Bunge amesema kuwa wataweka mambo sawa ili wabunge wawe na utulivu katika kusikiliza kazi za Bunge zinazoendelea.
“Huko Dar es salaam kuna zoezi linaendelea huko sasa kidogo kiti cha Spika kimetikiswa hivi tunatuhumiwa tuhumiwa hivi, tumeguswa guswa hivi kwahiyo natarajia kupata ushauri wenu kuona tunafanyaje katika mazingira haya maana kuna watoto wetu wako barabarani haiwezekani hata kidogo kwahiyo wakina mama wale inabidi tufanye utaratibu tujue nini tutafanya lakini kina baba wameendelea kujitokeza huko nimesikia na baadhi ya walalamikiwa ni wakina mama,” alisema Spika Ndugai.
“Wabunge kwahiyo hili jambo halina upande basi kama hao wamama wapo kweli basi waje kwa Spika au wamuandikie Spika lakini waniletee na DNA Test Certificate ili tuone namna gani kuwezesha tuna mafungu mafungu hapa tumepitisha tunaweza kuangalia namna gani tutaweka mambo sawasawa ili waheshimiwa wawe na utulivu katika kusikiliza kazi za Bunge na sio mambo mengine,” aliongeza.
Indadaiwa kuwa kati ya wanawake 480 waliosikilizwa 47 wamedai kutekelezwa na Wabunge.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: