Friday, 27 April 2018

SIMBA YATANGAZA VITA NA WANAHABARI


Na George Mganga 

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia Ofisa Habari wake, Haji Manara, umetangaza vita na Wanahabari watakaotumia neno MAHASIMU badala ya WATANi pindi wanapotangaza na kuziandika klabu hizo.

Manara ameeleza kuwa Simba na Yanga si mahasimu bali ni watani wa jadi, tofauti na baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikiripoti tofauti.

Manara ameyasema hayo leo alipotisha kikao na Waandishi wa Habari kwenye Makao Makuu ya Simba, yaliyopo Kariakoo.

Ofisa huyo wa Habari, amesema neno hilo lina maana mbaya ambayo ni VITA hivyo halipaswi kutumika huku akieleza kuwa wao si Palestina na Israel.

Kufuatia baadhi ya vyombo vya habari kuripoti wakizitaja timu hizo za Kariakoo kuwa ni Mahasimu badala ya watani wa jadi, Manara ametangaza kuwa klabu itaanzisha vita na Mwandishi au Mtangazaji yeyote atakayeripoti kwa kuandika ama kutamka jina la MAHASIMU badala ya watani wa jadi.

No comments:

Post a Comment