Tuesday, 24 April 2018

Rc Gambo: Familia nyingi zipo kwenye mateso makubwa


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amefunguka na kuwashauri wanaume wenzake kuacha tabia za kuwanyanyasa wake zao pindi wanapokuwa majumbani mwao kwa kuwafanyia vitimbi mbalimbali bila ya kufikilia kuwa mafanikio aliyokuwa nayo yametokana na mwenza wake huyo kwa namna moja ama nyingine.

Gambo ametoa nasaha hiyo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya kuwepo rundo la wanaume wenye chembechembe za tabia ya kuwaona si kitu wake zao pindi wanapokuwa wamepata mafanikio ya kimaisha na kusahau kuwa walianza pamoja harakati za kuomba Mungu awape mafanikio ya kimaisha.

"Familia nyingi zipo kwenye mateso makubwa sana kutokana na matendo ya wanaume ndani ya nyumba. Mwanamke mnaanza naye maisha, mnateseka naye mkiwa hamna chochote halafu Mungu anakupa riziki unaamua kumtesa mkeo. Wakati mwingine mwanaume unachukua hata chakula cha ndani (unga , mchele, sukari na nk) alichokihangaikia mkeo kwa ajili ya watoto wake na kupeleka nyumba ndogo", amesema Gambo.

Pamoja na hayo, Gambo ameendelea kwa kusema "nadhani haya mambo ni sababu kubwa za presha na sukari kwa familia nyingi. Wanaume ni busara kuheshimu nyumba yako hata kama una vituko vyako".

Kwa upande mwingine, Gambo amesema kuna hitajika tiba mbadala ya kuzisaidia familia zenye matatizo hayo kama taifa ili mradi kuweza kuwa wasaidizi wanawake waliolewa na wanaume wenye kadhia hiyo ambayo haipendezi mbele ya jamii wala kwa Mungu.

No comments:

Post a Comment