OmbaOmba Kutupwa Gerezani


Mamlaka katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali imetangaza kuanza msako mkali na kuwaweka gerezani walemavu wote wanaojihusisha na vitendo vya kuomba omba barabarani, kwa madai kuwa ni chanzo cha uchafu wa jiji hilo.

 Msako huo unaweza kutekelezwa wakati wowote kuanzia sasa, umewaonya walemavu hao kuwa kama hawataacha kuomba omba watakabiliwa na kifungo.

Baadhi ya wananchi wamepinga uamuzi huo wakisema, unalenga kukandamiza walemavu na watu masikini ambapo mashirika ya kiraia nchini Rwanda yameshauri kwamba kabla ya utekelezaji wa msako huo yafanyike mazungumzo ya pande zote.

Ripoti mbalimbali zimekuwa zikiitaja Kigali kuwa miongoni mwa majiji masafi barani Afrika huku ripoti nyingine hususani zile za kutetea haki za binadamu, zikiishutumu serikali kwa kuwafunga watu wasiojiweza.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: