Na.Ahmad Mmow.
JOPO la madaktari wa kutoka taasisi ya mifupa ya hospitali ya taifa Muhimbili(MOI) jana walianza kutoa huduma ya upasuaji kwa watoto wenye tatizo la vicwa vikubwa na migongo wazi katika hospitali ya wilaya ya Nachingwea,mkoa wa Lindi.

Akieleza mafanikio ya zoezi hilo ambalo lilianza hiyo jana(Jumamosi) nakutarajiwa kumalizika kesho(Jumatatu),mkuu wa wilaya ya Nachingwea,Rukia Muwangoa,alisema zoezi la upasuaji limeanza vizuri na wananchi wenye watoto wenye matatizo hayo wanaendelea kujitokeza.

Muwango alisema hadi wakati anazungumza na Muungwana(jina la blogi hii)watoto 15 walikuwa wamefanyiwa upasuaji.Huku wazazi na walezi watoto wengine wakipewa ushauri wa kitabibu na madaktari hao.

Alisema wataalamu hao pia watoa huduma kwa mtindo wa klinik kwa wagonjwa walioshindwa kwenda Muhimbili kwenye taasisi ya MOI kipindi kilichopita.

Mkuu huyo wa wilaya alibainisha kwamba katika wilaya hiyo na nje ya wilaya hiyo kunawatoto wengi wenye matatizo ayo.Kwahiyo alitoa wito kwa wazazi na walezi wa watoto wenye matatizo hayo wawapeleke wakapatiwe matibabu.

"Mimi naomba wajitokeze kwa wingi wapate huduma ya matibabu.Najisikia mwenye furaha kuona zoezi hili limefanikiwa na matibabu yanatolewa.Kwani mimi nimongoni mwa waliofanikisha upatikanaji wa huduma hii ambayo inatolewa katika hospitali hii kwa watoto wenye matatizo hayo wanaotoka katika mkoa wetu wa Lindi na mikoa ya jirani ya Mtwara na Ruvuma,"alisema Muwango.

Mbali na hayo,Muwango aliushukuru uongozi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili na MOI kwakukubali ombi lake la kwenda kutoa huduma hiyo na ushirikiano anaopata katika kufanikisha zoezi hilo kuanzia hatua za mwanzo hadi kufikia hatua ya hiyo.

Kwa mujibu wa taasisi ya MOI,inaonesha kuwa   theluthi moja ya  watoto 872 waliofanyiwa upasuaji mwaka uliopita walitoka katika mikoa ya Lindi na Mtwara.Ambapo watoto 10 kati ya 19 waliofanyiwa upasuaji hivi karibuni walitoka katika mikoa hiyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: