Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc leo April 4, 2018 Vodacom inapenda kuwataarifu wateja wake na Watanzania kwa ujumla kwamba, itaendelea kutoa huduma ya ununuzi wa umeme (LUKU) kupitia mfumo wa malipo wa serikali ujulikanao kama Government e-Payment Gateway (GePG).

Kufuatia mabadiliko yaliyotangazwa hivi karibuni na kampuni ya kuzalisha na kutoa huduma ya umeme nchini (TANESCO) kuhusu kuanza kutoa huduma ya kununua umeme kwa kupitia mfumo wa Serikali wa GePG, Vodacom Tanzania Plc inapenda kuwatoa hofu Wateja wake kwamba wataendela kupata huduma ya kununua umeme ya LUKU kupitia Vodacom M-Pesa kama ilivyokuwa mwanzo.

Mfumo mpya utaiwezesha TANESCO kuunganisha mauzo moja kwa moja kutoka makampuni mengine ya simu na mabenki kwenda GePG ikiwa ni matakwa ya sheria kwa taasisi za Serikali.

Kutakuwa na ongezeko la asilimia moja nukta moja ya gharama halisi (1.1%) anayotozwa Mteja ili kununua umeme pindi atumiapo huduma ya M-Pesa. Vodacom inawahakikishia Wateja wake kwamba itaendelea kutoa huduma ya LUKU kupitia M-Pesa 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: