Tuesday, 10 April 2018

Breaking : BASI LA KAMPUNI YA MAQADIR LAPATA AJALI TANGA


Muonekano wa ajali hiyo baada ya basi hilo kuanguka katikati ya barabara.

Basi la Kampuni ya Maqadir lililokuwa linatoka jijini Tanga kwenda Kijiji cha Mtae, Wilaya ya Lushoto mkoani humo, limeanguka asubuhi  leo Aprili 10, 2018 katikati ya barabara kuu ya Segera-Tanga katika kijiji cha Mpakani, kata ya Kerenge wilayani Muheza mkoani Tanga.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, majeruhi wa ajali hiyo ni mmoja na bado hajatambuliwa ambapo  chanzo cha ajali hiyo, pia bado hakijafahamika.

No comments:

Post a comment