Friday, 27 April 2018

Boti yapinduka Ziwa Victoria

Watu wawili wamefariki dunia baada ya boti waliyokuwa wakitumia kusafiria kupinduka. Ilipokumbwa na dhoruba kali katika ziwa Victoria, Sengerema jijini Mwanza.

Akizungumza na www.eatv.tv kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, amesema boti hiyo ilikuwa na jumla ya watu watano ambao walikuwa wa wakisafiri kutoka Sengerema kuja Mwanza, na ndipo ilipokumbwa na dhoruba wakiwa njiani, na kusababisha boti hiyo kupinduka na watu hao kufariki.

“Kuna boti ilikuwa inatoka Sengerema kuja huku Mwanza, ilikuwa imebeba mkaa pamoja na udaga, walivyokwenda kama robo safari yao hali ya hewa ikawa mbaya kukawa na dhoruba, wakiwa wanageuza wanarudi ikawa shida ikapinduka, ndani ya hiyo boti kulikwa na watu watano, wanaume wanne mwanamke mmoja, watatu waliweza kuogelea lakini hawa wawili walishindwa, mwanamke na mwanaume mmoja, majina bado sijayapata”, amesema Kamanda Msangi.

Kamanda Msangi amesema miili ya watu hao imepatikana, na wanafanya utaratibu wa kuihifadhi hospitali, ili ndugu waweze kuitambua na kuichukua kwenda kuzika.

No comments:

Post a Comment