BARAZA la Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, limemtenga Askofu wake wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk. Alex Malasusa, kwa tuhuma za usaliti.


Taarifa za uhakika ambazo gazeti la Mtanzania limezipata, zinasema uamuzi wa kumtenga Askofu Malasusa ulifikiwa usiku wa kuamkia juzi na kikao cha Baraza la Maaskofu wapatao 25 lililoketi mjini Arusha, chini ya kiongozi wake ambaye ndiye Mkuu wa kanisa hilo, Askofu Dk. Fredrick Onael Shoo.

Kwa mujibu wa Taarifa hizo uamuzi huo wa kumtenga Askofu Malasusa ulitangazwa pia kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya
KKKT cha siku mbili ambacho nacho kilikuwa kikifanyika mkoani Arusha na kuhudhuriwa na wajumbe wake ambao ni Maaskofu, Makatibu Wakuu wa Dayosisi zote pamoja na wakuu wa vitengo.

Kiini cha tuhuma hizo za usaliti dhidi ya Askofu Malasusa, kinaelezwa kuwa ni uamuzi wake wa kuzuia waraka wa Pasaka ulioandaliwa na Maaskofu 27 wa Kanisa hilo, usisomwe katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani anayoiongoza.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti hili limezikusanya toka katika vyanzo mbalimbali ndani ya kanisa hilo na kikao ambacho kimemtenga Askofu Malasusa ambaye amekuwa Mkuu wa Kanisa hilo kwa miaka mingi, Baraza hilo liliona uamuzi huo kama hujuma dhidi ya Mkuu wa Kanisa wa sasa lakini pia usaliti na uchonganishi kati ya kanisa hilo na watu walio nje.

“Ni kweli kwamba ametimuliwa kwenye nyumba ya maaskofu kwa kosa la usaliti, hatukupiga kura tuliamua kwa sauti ya pamoja, yeye wakati waraka ule wa Pasaka tunauandaa hakuwepo, lakini alipigiwa simu na akasema tupo pamoja, ulipotoka akaagiza usisomwe, ujumbe wa kutaka waraka huo usisomwe ulisambazwa na msaidizi wake kwa wachungaji wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani na haukusomwa.

“Huu ni usaliti kwa Maaskofu na Kanisa, Baraza la Maaskofu limetafakari na kubaini hii si mara ya kwanza kwenda kinyume na
maamuzi ya baraza, sasa sisi tunasema hili ni kosa linachonganisha kanisa,” kilisema chanzo chetu.

Ujumbe ambao Askofu Malasusa anatuhumiwa kumwagiza mmoja wa wasaidizi wake autume kwa wachungaji wa Dayosisi anayoiongoza ukiwazuia wasiusome waraka huo siku ya Jumapili ya Pasaka unasomeka hivi:-

Bw. Yesu asifiwe Viongozi. Tafadhali mnaombwa kuwajuza Watumishi wote katika majimbo yenu kuwa inaelekezwa kwamba araka wa Pasaka kutoka KKKT usisomwe wala kutajwa katika ibada au popote hadi hapo uongozi wa Dayosisi utakapotoa maelekezo.

limezipata, zinasema uamuzi wa kumtenga Askofu Malasusa ulifikiwa usiku wa kuamkia juzi na kikao cha Baraza la Maaskofu wapatao 25 lililoketi mjini Arusha, chini ya kiongozi wake ambaye ndiye Mkuu wa kanisa hilo, Askofu Dk. Fredrick Onael Shoo.

Kwa mujibu wa Taarifa hizo uamuzi huo wa kumtenga Askofu Malasusa ulitangazwa pia kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya
KKKT cha siku mbili ambacho nacho kilikuwa kikifanyika mkoani Arusha na kuhudhuriwa na wajumbe wake ambao ni aaskofu, Makatibu Wakuu wa Dayosisi zote pamoja na wakuu wa vitengo.

Kiini cha tuhuma hizo za usaliti dhidi ya Askofu Malasusa, kinaelezwa kuwa ni uamuzi wake wa kuzuia waraka wa Pasaka ulioandaliwa na Maaskofu 27 wa Kanisa hilo, usisomwe katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani anayoiongoza.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti hili limezikusanya toka katika vyanzo mbalimbali ndani ya kanisa hilo na kikao ambacho
kimemtenga Askofu Malasusa ambaye amekuwa Mkuu wa Kanisa hilo kwa miaka mingi, Baraza hilo liliona uamuzi huo kama hujuma dhidi ya Mkuu wa Kanisa wa sasa lakini pia usaliti na uchonganishi kati ya kanisa hilo na watu walio nje.

“Ni kweli kwamba ametimuliwa kwenye nyumba ya maaskofu kwa kosa la usaliti, hatukupiga kura tuliamua kwa sauti ya pamoja, yeye wakati waraka ule wa Pasaka tunauandaa hakuwepo, lakini alipigiwa simu na akasema tupo pamoja, ulipotoka akaagiza usisomwe, ujumbe wa kutaka waraka huo usisomwe ulisambazwa na msaidizi wake kwa wachungaji wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani na haukusomwa.

“Huu ni usaliti kwa Maaskofu na Kanisa, Baraza la Maaskofu limetafakari na kubaini hii si mara ya kwanza kwenda kinyume na
maamuzi ya baraza, sasa sisi tunasema hili ni kosa linachonganisha kanisa,” kilisema chanzo chetu.

Ujumbe ambao Askofu Malasusa anatuhumiwa kumwagiza mmoja wa wasaidizi wake autume kwa wachungaji wa Dayosisi anayoiongoza ukiwazuia wasiusome waraka huo siku ya Jumapili ya Pasaka unasomeka hivi:-

Bw. Yesu asifiwe Viongozi. Tafadhali mnaombwa kuwajuza Watumishi wote katika majimbo yenu kuwa inaelekezwa kwamba waraka wa Pasaka kutoka KKKT usisomwe wala kutajwa katika ibada au popote hadi hapo uongozi wa Dayosisi utakapotoa maelekezo. CC-ASKOFU, DEAN, KM

Taarifa zinaeleza kuwa katika kikao hicho, Askofu Malasusa, alipewa nafasi ya kujitetea na katika maelezo yake akasema aliona tayari waraka huo umesambaa vya kutosha kwenye mitandao ya kijamii na hivyo kuamini kuwa umekwishawafikia waumini wote.

Inaelezwa kuwa alipoulizwa kuhusu ujumbe anaotuhumiwa kuagiza utumwe kwa wachungaji ukiwakataza kuusoma waraka huo, Askofu Malasusa, alijibu kuwa si wake na kutaka aulizwe aliyeutuma.

Pamoja na Askofu Malasusa kutoa maelezo hayo, inaelezwa kuwa baadhi ya wachungaji wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ndio waliopeleka kwenye Baraza la Maaskofu vielelezo vya barua wakiwa wamezisaini na kuthibitisha walipewa maelekezo ya kutousoma waraka huo.

Inaelezwa kuwa hoja hizo za Malasusa hazikuliridhisha Baraza la Maaskofu na hivyo kutangaza kumtenga na kwa sababu hiyo sasa hatahudhuria kikao chochote cha baraza hilo wala maamuzi yake hayatamgusa.

Zaidi inaelezwa kuwa ameondolewa kwenye kamati zote alizokuwa akiziongoza na haruhusiwi kuliwakilisha kanisa hilo mahali
popote.

Chini ya utaratibu wa Kanisa hilo, inaelezwa kuwa pamoja na kwamba Kanisa linaongozwa na Baraza la Maaskofu, lakini uamuzi wa kumvua uaskofu Dk. Malasusa uko chini ya Dayosisi anayoingoza ya Mashariki na Pwani.

“Ataendelea kuwa Askofu lakini hatahudhuria kikao chochote wala maamuzi yoyote ya Baraza la Maaskofu hatahusika nayo, na
amepewa muda wa kutafakari kuhusu uamuzi huo hadi Septemba mwaka huu na kisha arudi kuliomba radhi kanisa … sasa ni jukumu la Dayosisi ya Mashariki na Pwani kuona kama ni sahihi kuendelea au la na Askofu aliyetengwa na Baraza la Maaskofu.” Kilisema chanzo chetu kingine ndani ya Kanisa hilo.

MTANZANIA Jumamosi jana liliwasiliana kwa njia ya simu na Askofu Malasusa ili kufahamu ameupokeaje uamuzi huo, lakini alimtaka mwandishi wetu kuwasiliana kwa namba ya ofisini kwake na si yake binafsi.

Mwandishi alipomweleza kuwa namba hiyo ni imekuwa ni vigumu kumpata alisema kuwa muda huo wakati akipigiwa simu saa sita mchana alikuwa kwenye kikao na kisha akakata simu.

Gazeti hili liliwasiliana na Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Godfrey Nkini, ambaye hakukubali wala kukana juu ya kuwako kwa taarifa hizo na kumwelekeza mwandishi wa habari hizi awasiliane na Katibu Mkuu wa KKKT, aliyemtaja kwa jina la Brighton Killewa.

“Anayepaswa kuzungumzia jambo hilo ni Katibu Mkuu wa KKKT anaitwa Killewa, yupo Arusha, mtafute huyo,” alisema Nkini.

Alipotafutwa Killewa kupitia simu yake ya kiganjani naye alimwelekeza mwandishi wa habari hizi kumtafuta kiongozi wa Kanisa hilo, Askofu Dk. Shoo.

Askofu Dk. Shoo alipotafutwa mara kadhaa kupitia simu yake ya kiganjani hakupokea na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi hakujibu. Gazeti hili linaendelea kumtafuta.

Mmoja wa maofisa wa kanisa hilo aliyekuwamo katika kikao kilichofikia uamuzi wa kumtenga Dk. Malasusa, alilithibitishia gazeti hili taarifa hizo ingawa alisema yeye si msemaji.

Waraka huo wa Pasaka ambao unadaiwa kumponza Askofu Malasusa, ni ule uliotolewa na kusainiwa na maaskofu 27 wa kanisa hilo, akiwamo Askofu huyo mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu wiki moja kabla ya maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka.

Waraka huo ambao pamoja na mambo mengine uligusa na kuonya mwenendo wa masuala ya uchumi, siasa na kijamii, uliamsha
mjadala mkali ndani ya jamii, viongozi wa Serikali na kisiasa na hata kumwibua Rais Dk. John Magufuli.

Mijadala na malumbano na pengine iliyoonekana kuchagiza kauli za baadhi ya viongozi wa kisiasa na Serikali kuhusiana na waraka huo, iliwafanya baadhi kukumbuka waraka ule uliotolewa mwanzo na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini TEC, uliotolewa Februari 9 mwaka huu ukiwa ni ujumbe wa Kwaresma chini ya kauli mbiu “Basi enendeni mkawafanye
mataifa yote kuwa wanafunzi wangu: Mt.28:19.”

Ni waraka huo na ule uliokuja baadaye wa maaskofu 27 wa KKKT, ndio uliotajwa na pengine kujenga hisia kwa baadhi kuwa nyuma ya kauli ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo, ambaye alilitumia kongamano la vijana lililofanyika Bagamoyo katika wiki hiyo hiyo ya kuelekea Pasaka kuupinga, akisema viongozi wa dini hawapaswi kuchanganya siasa na kazi yao ya kitume.

Siku moja baadaye baada ya waraka huo wa KKKT kutolewa, Rais Dk. Magufuli, katika hafla ya uzinduzi wa magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) aliwaomba maaskofu na viongozi wengine wa dini kuhubiri ujenzi wa viwanda vya dawa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, katika andiko lake lililosambazwa kwenye mitandao ya kijamii alitumia mafumbo na mifano mingi kuchambua yale yaliyoandikwa kwenye waraka huo.

Waraka huo wa KKKT ambao uliandaliwa na maaskofu 27 akiwamo Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Fredrick Shoo, ulichambua masuala ya jamii, uchumi, maisha ya siasa, umuhimu wa Katiba Mpya na matukio yaliyo kinyume na kile walichokiita tunu na misingi ya Taifa.

Katika eneo la uchumi waraka huo wa KKKT ulionya kile ilichokiona kuwako kwa dhana ya Serikali kutaka kushindana na wadau wa maendeleo, lakini pia mfumo usio sahihi wa ukusanyaji kodi na ambao unafilisi wafanyabiashara.

Kuhusu siasa, waraka huo ulikumbusha misingi ya siasa safi na uongozi bora na kuonya Serikali kuminya demokrasia ya vyama vingi, uhuru wa Bunge na vyombo vinavyotoa na kusimamia haki kama Mahakama na Tume ya Uchaguzi.

Zaidi ulizungumzia dhana ya kile kinachodhaniwa baadhi ya wanasiasa kununuliwa na gharama za kurudia uchaguzi huku katika
suala la ajira kwa vijana ukitaka jitahada za wazi zifanyike na kuonya elimu kuchokonolewa.

Waraka huo ulishauri suluhisho la yote hayo ni upatikana kwa Katiba Mpya ambayo ina maoni ya wananchi na kupendekeza suala hilo lifanyike kabla ya uchaguzi wa mwakani.

Chanzo- Mtanzania
Share To:

msumbanews

Post A Comment: