Thursday, 19 April 2018

BABU SEYA, FAMILIA YAKE WATINGA BUNGENI – PICHAMWANAMUZIKI nguli wa dansi, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na watoto wake ambao ni Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ na Francis Nguza, leo Alhamisi, Aprili 19, 2018 wametembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodomabaada ya kualikwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mariam Ditopile.

Babu Seya na familia yake, walishangiliwa na Bunge zima baada ya kutambulishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai,   baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika bungeni humo.

Wanamuziki hao walikuwa ni miongoni mwa wafungwa 8,157 waliosamehewa na Rais John Magufuli siku ya maadhimisho ya sherehe za uhuru wa Tanganyika, Desemba 9, 2017 zilizofanyika mjini Dodoma.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: