Saturday, 14 April 2018

Baba Levo ampiga Daktari kisha kutoweka kusikojulikana

Diwani wa Kata ya Mwanga Kaskazini  Mkoani Kigoma Revokatus Kipando maarufu kwa jina la Baba Levo amemdhalilisha kwa kumpiga Dk. wa Zahanati ya  Msufini iliyoko mkoani kigoma   kwa kosa la kuchelewesha kuwalipa vibarua waliokua wanafanya ukarabati katika zahanati  hiyo.

Daktari huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema diwani alifika nakuanza kumdhalilisha na kumkashifu kwa kuchelewesha kuwalipa wafanyakazi hao  mbele ya wagonjwa  na kusababisha wagojwa kuondoka pasipo kutibiwa.

“Amefika  hapa kwa kufoka, kunitukana , kufanya vurugu ofisini na kanipiga, kisa pesa zilizo nje ya uwezo wangu ambazo zilikua na utaratibu za kufuatiliwa lakini hataki kufuata taratibu za kazi amehatalisha amani ya maisha yangu  na hii siyo mara ya kwanza na yuko kinyume cha sheria,” alisema Daktari huyo.

Kwa mjibu wa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo  Muuguzi wa Hospitali wa zamu  ambaye jina lake limehifadhiwa  alisema Diwani huyo malufu kama baba   alifika katika zahanati hiyo  na kuanza  kumfokea  Daktari huyo kisha kumpiga.


 Kwa  upande wake Diwani huyo wa Mwanga Kasikazini  maarufu kama Baba Levo amekana kufanya kitendo hicho cha udhalilishaji kwa Daktari  mpaka sasa Jshi la Polisi mkoani Kigoma linamsaka mtuhumiwa huyo ili kujibu mashitaka yanayo mkabili
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: