Kufuatia sintofahamu iliyoibuka hivi karibuni kuhusu suala la michango mashuleni, Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William OleNasha ametoa ufafanuzi wa kisera juu ya jambo hilo.

Ole Nasha amesema michango yote mashuleni iratibiwe na ofisi za wakurugenzi wa halmashauri husika lakini pia isitokee michango hiyo ikafungamanishwa kwa aina yoyote na mwanafuzi.

Katika kuwapunguzia wazazi mzigo wa michango mashuleni serikali ilipitisha uamuzi wa kupitiwa upya na kuratibiwa vyema utaratibu wa michango yote mashuleni, ambapo uamuzi huo unaonekana kuibua sintofahamu katika baadhi ya maeneo nchini.

Akiwa mkoani Kilimanjaro, katika halfa za kutia wakfu jina jipya la shule ya sekondari Bishop Alpha Mohamed High school kutoka jina la zamani Pasua Sekondari, Olenasha alitoa ufafanuzi huo wa Serikali.

Pamoja na kutiwa wakfu kwa jina jipya la shule hiyo ,waumini wa kanisa la Anglican,wachungaji ,maaskofu na viongozi wa kisiasa na serikali walifanya Harambee ya kuchangisha fedha za kumalizia ujenzi wa bwalo la shule hiyo,huku Askofu wa kanisa hilo Tanzania Dayosisi ya Maunti Kilimanjaro Dar.Stanly Hotay akitoa wito kwa serikali kushirikiana katika uratibu na utoaji wa elimu kupitia shule binafsi

Katika Harambee hiyo kiasi cha shilingi milioni 58 kilipatikana hii ikijumlisha ahadi na fedha taslim,ambapo wizara ya elimu pekee ilichangia shilingi milioni nane.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: