Waziri Nchemba atoa msaada wa mabati kusaidia ujenzi wa mabweni


Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi  Dr Mwigulu Nchemba ametoa mabati 210 na cement mifuko 100 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati na mabweni ya wanafunzi katika kata ya Mtoa kusaidia kupunguza hadha wanayopata wananchi ambao inawalazimu kuvuka mto mkubwa kufata huduma ya afya umbali wa zaidi ya kilimota 10.

Waziri Nchemba amesema anakwelwa na jengo kukaa mda mrefu bila kumaliziwa hivyo ameamua kutoa bati 210 na kuchangia shilingi milioni moja na nusu kwa ajili ya ununuzi wa mbao ili ujenzi uanze mala moja na kikamilike ndani ya mwaka huu kianze kutoa huduma.

Dr Nchemba amesema  hayo akiwa ziarani katika kata ya Mtoa kijiji cha Masiga kitongoji cha kisaki jimboni kwake iramba Magharibi mkoa wa Singida  kutekeleza ahadi alizozitoa wakati anagombea mwaka 2015.

Aliongeza kusema kuwa wakati wa masika kama huu baadhi ya maeneo ni ngumu sana hata magari kufika kutokana  mito kujaa maji na barabara kuwa na utelezi na kufanya gari au watu kushindwa kupita kufata huduma hivyo ameamua kutoa mifuko 100 yaa cement ili ujenzi wa bweni la shule ya sekondari mtoa likamalike kuwasaidia wanafunzi ambao wanaishi mbali wawwze kujisomea vizuri kuliko sasa hadha wanayopata kuvuka mito ambapo ni hatari.

"Mimi nakelwa na jengo kukaa mda mrefu hivi,hatulali hata sekunde tunaendelea kutafuta mbao na bati nyingi zikafunike baadhi ya vituo kwahiyo ninapoona jengo lipo hivi wala mtu asidhanie nafurahie jengo libaki vilee"alisema Dr Mwigulu

Nao wananchi wa kata ya mto awamemshukuru mbunge wao kwa kuwaletea mabati na cement kwa ajili ya kumalizia zahanati yao ya mtoa kwani ni jambo ambalo walikuwa wanalilia kupata zahanati hiyo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: