Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole, ametoboa siri ya CCM kushindwa mara mbili mfululizo uchaguzi Jimbo la Mbeya Mjini ambalo linaongozwa na Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na kusema kwamba Ubaguzi ndiyo chanzo cha mambo yote.
Polepole amesema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM ngazi mbalimbali wilaya ya Mbeya Mjini, ambapo amefafanua kwamba siasa za makundi na ubaguzi wa kikabila zimekuwa zikiikosesha CCM ushindi kwenye jimbo hilo la Mbeya.
Kiongozi huyo ameongeza kwamba tatizo hilo lilibainika wakati uongozi wa juu ulipofanya tathmini ya majimbo ambayo CCM haikushinda kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, likiwamo jimbo hilo ambalo ni ngome ya CHADEMA pia yenye madiwani wengi.
Amefafanua kuwa ubaguzi huo umekuwa ukiifanya CCM kuonekana nyonge/dhaifu  mbele ya wapinzani na hivyo kukosa hoja kwenye uchaguzi pamoja na kuwapa faida wapinzani.
Siasa za ubaguzi wa kikabila haziwezi kutufikisha popote, haijalishi kiongozi huyo anatoka kabila gani, cha msingi awe anashughulikia changamoto za wananchi. Viongozi fanyeni kila linalowezekana kuondoa tatizo hilo, ili tushinde kwenye chaguzi zijazo" .
Polepole amesema ubaguzi wa aina hiyo ni wa miaka mingi hivyo akawataka viongozi wa chama hicho kuhakikisha wanaondoa changamoto hiyo haraka, ili kufanikisha ushindi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani na Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: