Wednesday, 28 March 2018

Rungwe aliomba Jeshi la Polisi kusaidia upatikanaji wa ndugu zake


Mwanyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) Hashim Rungwe ameliomba jeshi la polisi kusaidia upatikanaji wa Mpwa wake Saida Hilal (40) na mumewe Abdallah Kutiku ambao hawajaonekana tangu Machi 26, 2018 majira ya asubuhi.

Hashim Rungwe amesema hayo leo Machi 27, 2018 na kudai Saida Hilal aliaga wenzake ofisini na kwenda kituo cha polisi kufuatilia suala la mume wake Abdallah Kutiku ambaye alichukuliwa na polisi

"Huyu binti alikuwa anafuatilia habari za mumewe polisi kwa kuwa mumewe alikuwa amekamatwa na polisi hivyo naye hapatikani kwa hiyo wote wawili hawaonekani kwani tulipofika kituo cha polisi walisema hawa watu hatuwafahamu na wala hawajafika pale, tangu hapo Bi. Saida Hilal hapatikani kwenye simu zake na tumefanya jitihada kumtafuta kwenye vituo vya polisi na mahospitali kama Muhimbili, Mwananyamala na sehemu zingine za usalama bila mafanikio"

Rungwe aliendelea kuelezea kuwa "sehemu zote ambazo alikuwa anapenda kutembelea zote tumepita na hatujafanikiwa, tunaomba vyombo vya dola watusaidie kuwatafuta hawa wote na kama wanawashikilia kwa mujibu wa sheria tungeomba tufahamu ili iweze kutuondolewa hofu kubwa tuliyonayo, tunahofu kubwa juu ya kutoonekana huyu binti maana ana watoto watano alitoka asubuhi nyumbani kwake na kwenda kazini yeye anafanya kazi Tume ya Uchaguzi, kazini kwako haonekani na watu wa kazini wamejitahidi kumtafuta wamekwama

No comments:

Post a comment