JUMLA ya wanachama 27 kutoka Chama cha NCCR-Mageuzi  akiwemo aliewahi kuwa Diwani Kupitia Chama hicho Kata ya Kitagata  wilayani Kasulu mkoani Kigoma wamejiunga CCM.Miongoni mwa hao walijiunga CCM wapo pia wanaotoka Kata ya Nyakitonto na wamefikia uamuzi kutokana na utendaji kazi unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.

Wanachama hao wapya wamejiunga CCM leo mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Humphray Polepole ambaye yupo mkoani Kigoma akikagua  utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2015-2020.Wakizungumzungumza  mara baada ya kujiunga na CCM, wachama hao wamesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona kazi inayofanywa na uongozi wa awamu ya tano na viongozi wanavyozunguka kutatua kero za wananchi na kuchochea Maendeleo na kuinua uchumi wa wananchi.

Damiani Cosmasi ambaye aliwahi kuwa Diwani kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi amesema yeye amekuwa kiongozi katika chama hicho na hajawahi ona viongozi wa chama hicho  kufika kuwatembelea na kuwasaidia katika masuala ya maendeleo.Pia amesema wanapowachagua viongozi  hawawaoni hadi hapo wanapoanza kuomba kura tena ndipo wananza kuwatembelea.

Amesema Serikali ya CCM imejitahidi kuyafanyia kazi yale yote yaliyo ahidi wakati wa kampeni na wameanza kuona mabadiliko na maendeleo mpaka vijijini. "Kila mtu ni lazima amuunge mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania kutokana na kazi kubwa anayoifanya ya kuwahudumia wanyonge ambapo ndicho kilicho kuwa kilio cha wananchi wengi," amesema.

Akizungumza baada ya kushiriki ujenzi wa Shule ya Msingi  Kasasa Kijiji cha Kasasa kata ya Kitagata a Wilaya ya Kasulu  na wananchi wa Kijiji hicho, Polepole amesema Serikali imeamua kuwasaidia wananchi kuwatoa katika dimbwi la umasikini na kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na shule na wanafunzi wote wanaofikia umri wa kwenda shule waende kama Ilani ya CCM  inavyoeleza.

Amesema kwa kazi kubwa inayofanywa na CCM na Serikali hiyo ni lazima wananchi wakubaliane nae kwakuwa anachokifanya  ndilo lililokuwa hitaji la wananchi wengi."Na Serikali imeandaa fedha nyingi kwaajili ya kuinua uchumi wa wananchi na kuhakikikisha wanaondokana na umasikini kupitia miradi ya maendeleo inayoanzishwa na Serikali ya CCM.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: