Ngorongoro Heroes kusaka tiketi ya AFCON leo

Kikosi cha timu ya taifa chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes kinashuka Uwanja wa Taifa kukabiliana na Congo (U20) katika mchezo wa kwanza wa kufuzu kutafuta tiketi ya kushiriki mashindano ya AFCON (U20).

Ngorongoro itakuwa inacheza mechi yake ya kwanza kabla ya kurudiana na Congo bada ya wiki mbili huko Kinshasa nchini humo.

Kocha wa kikosi hicho, Ammy Ninje, amesema tayari vijana wameshajiandaa na wapo kamili kwa ajili ya pambano hilo dhidi ya wapinzani wao.

Mchezo huo unataraji kuanza majira ya saa 10 kamili jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: