Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk Charles Tizeba na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina pamoja na Makatibu wao wameshindwa kuhudhuria mkutano wa 11 wa baraza la taifa la Biashara uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuendeshwa na Rais Dkt Magufuli

Kufuatia kutokuwepo Rais Magufuli alimuuliza Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kama waliweza kuwaalika mawaziri hao na ndipo Waziri Mkuu alipojibu kuwa walipata mwaliko na walipaswa kuwepo kwenye mkutano huo ingawa hakukuwa na taarifa yoyote wao kutokuwepo wala kutuma wawakilishi wao. 
"Kwa hiyo wa Kilimo na Mifugo mawaziri na Makatibu wakuu wote hawapo? Wao sio wajumbe wa mkutano huu? Alihoji Rais Magufuli ndipo Mawaziri Mkuu aliibuka na kutoa majibu kwa Rais Magufuli. 
"Mawaziri wote wanaoguswa na sekta za uwekezaji na kusupport uchumi wetu wa viwanda, kilimo ni facilitater wa viwanda na Mifugo naye pia ni wa viwanda walikuwa wapaswa kuwepo hapa kwa sababu walishapewa taarifa wote" 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: