Friday, 23 February 2018

Waziri Ndalichako : Kumsomesha mdogo wake AkwilinaWaziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako ameahidi kumsomesha mdogo wake Akwilina Akwilini, Angela Akwilini ambaye kwa sasa anasoma kidato cha tatu.
Akizungumza na mamia ya waombolezaji baada ya kumalizika kwa ibada ya mazishi iliyofanyika kanisa la Mtakatifu Theresia Parokia ya Olele , Profesa Ndalichako amesema atamsomesha Angela hadi Chuo Kikuu.
Mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini umezikwa nyumbani kwa wazazi wake kijiji cha Olele wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.No comments:

Post a comment