Wastara
Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Wastara ameondoka nchini kuelekea India kwa ajili ya matibabu ya mguu wake ulioanza kumsumbua mwishoni mwa mwaka jana huku akiwashukuru watanazania na Vyombo vya Habari kwa kuwa pamoja naye kipindi alivyokuwa akihitaji msaada wa fedha.
Wastara akiongea na waandishi wa Habari mapema leo Jumapili Februari 4, 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam, amesema “nina washukuru sana vyombo vya habari wote kwa moyo wa upendo walionesha kwa sababu bila ya wao hata mimi nisingekuwa Wastara. Napenda kuwaambia watanzania kwamba tuamini sana maneno anayosema mtu kuliko neno analosema mtu mwingine kwa hiyo naamini kuna wengine watakuja na matatizo tujaribu kuwaangalia nawao pia”. 
Na alipoulizwa kuhusu tuhuma za kutumia fedha za matibabu kwa starehe kama alivyowahi kuchangiwa kipindi cha nyuma na kwenda Dubai, Wastara amesema hajawahi kuchangiwa na Watanzania bali alisaidiwa Makamu wa Rais na hakutumia kwa matumizi mengine.
Kwanza niseme sijawahi kuchangiwa na Watanzania mimi kama mimi, mara ya kwanza nilipoumwa aliyenichangia asilimia kubwa alikuwa ni Makamu wa Rais, na uzuri ni kwamba mpaka nafika hospitalini nilikuwa nampigia simu. Kilichosababisha watu waseme baada ya kufika hospitali kama hivi ninavyokwambia wiki tatu linapotokea tatizo kama umefanyiwa Oparesheni au upasuaji wowote niliambiwa unauwezo wa kukaa au kuishi kwenye hoteli karibu na hospitali..Ndipo watu wa karibu yangu wa Oman wakawa wamenipa Visa nikaenda kukaa huko kwa muda.“ameongea Wastara.
Share To:

Post A Comment: