Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Ushindi huo wa Simba unaifanya sasa timu hiyo kufikisha alama 38 kileleni mwa msimamo wa ligi na kuziacha Azam FC katika nafasi ya pili ikiwa na alama 33 huku Yanga ikiwa katika nafasi ya tatu na alama 31.
Mabao ya Simba leo yamefungwa na John Bocco mawili katika dakika za 24 na 66 pamoja na Mzamiru Yassin dakika ya 76. Moja ya tukio ambalo limetokea kwenye mchezo wa leo ni mlinzi wa Ruvu Shooting Mau Bofu kumpiga kiwiko Emmanuel Okwi, tukio ambalo lilisababisha Bofu kuoneshwa kadi nyekundu.
Kwa upande wa John Bocco sasa amefikisha mabao tisa akiwa nyuma ya Emmanuel Okwi mwenye mabao 12 katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu. Mchezo unaofuata wa Simba utakuwa dhidi ya Azam FC.
Share To:

Post A Comment: