Wanaharakati wamburuza mahakamani Rais Kenyatta


Wanaharakati nchini Kenya wamefungua kesi mahakamani kupinga baraza la mawaziri katika serikali ya Uhuru Kenyatta kwamba liliundwa kinyume cha Katiba ya nchi hiyo.
Wanaharakati hao wanataka baraza hilo livunjwe kwa sababu halikufuata maelekezo ya katiba ya nchi hiyo kwamba angalau theluthi moja ya mawaziri wawe wanawake.
Aidha, Kesi hiyo inawajumuisha mwanasheria mkuu wa Kenya, katibu wa baraza la Mawaziri na bunge la nchi hiyo kwa kutofuata utaratibu.
Wanaharakati hao wanataka mahakama hiyo kuamuru kuvunjwa kwa hatua ya bunge la taifa ya kuidhinisha uteuzi wa mawaziri hao kwakuwa ilienda kinyume na katiba ya nchi hiyo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, uteuzi katika utumishi wa umma unatakiwa kutilia maanani kipengele kuhusu usawa wa jinsia, ambapo si halali kwa raia wa jinsia moja kuchukua zaidi ya theluthi mbili ya nafasi za 
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: