Ofisa usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) Mkoa wa Manyara, Emmanuel Joshua akizungumza leo Februari 24,2018 amesema baada ya hatua ya kwanza ya usajili kumalizika, kinachofanyika ni kuchukua alama za vidole na kuwapiga picha wachimbaji hao.
Joshua amesema wachimbaji wengi wamejitokeza kujisajili, kazi inayofanyika kwenye machimbo hayo eneo la kitalu B (Opec) na kitabu D.
Amesema wana wafanyakazi wa kutosha wenye uwezo wa kufanya kazi ipasavyo ili kuhakikisha hakuna vikwazo vinavyojitokeza.
Mmoja kati ya wachimbaji hao, Bakari Baina amesema usajili utakuwa na manufaa kwao kwa kuwa ni haki yao ya msingi kupatiwa vitambulisho vya Taifa.
Baina amesema hata wale wenye kusita kushiriki wanapaswa kujitokeza kwa kuwa mwisho wa siku watashindwa kujulikana wao ni raia wa nchi gani.
Post A Comment: