Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF leo limeweka wazi kuwa Rais wa FIFA Gianni Infantino alisisitiza kuwa lazima shirikisho lipinge masuala ya rushwa michezoni kwenye mkutano wa (FIFA Football Executive Summit) uliofanyika nchini.

''Rais wa FIFA Gianni Infantino, akiwa kwenye mkutano wa FIFA nchini Februari 22 aliacha ujumbe mkubwa akisisitiza kupingana na masula ya rushwa'', wameandika TFF kupitia tovuti yao.

TFF pia wameongeza kuwa moja ya mambo aliyoyaacha Infantino ni kufurahishwa kwa namna Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF linavyoendeshwa kwa uwazi kwenye masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya fedha.

Aidha TFF pia imethibitisha kuwa moja ya mada ambazo Infantino alizijadili ni pamoja na kuanzishwa kwa ligi kubwa ya wanawake nchini.

Mkutano wa FIFA ulifanyika Februari 22, 2018 na kushirikisha jumla ya mashirikisho 21 ya mpira ambao ni wanachama wa shirikisho hilo na Ajenda kubwa ilikuwa kujadili namna ya kukuza soka la wanawake,soka la vijana na suala la usajili kwa njia ya mtandao.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: