TFF yakagua uwanja ligi ya wanawake - MSUMBA NEWS BLOG

Friday, 23 February 2018

TFF yakagua uwanja ligi ya wanawake


Shirikisho la soka nchini TFF kupitia kwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kutoka Kanda namba 5 ya mikoa ya Kigoma na Tabora, Issa Mrisho Bukuku imekagua uwanja wa Lake Tanganyika.
Uwanja huo umekaguliwa kwaajili ya kutumika katika mchezo wa ufunguzi wa hatua ya nane bora ya Ligi ya wanawake nchini ambao utazikutanisha timu za Kigoma Sisters na Simba Queens utachezwa Februari 25, 2018.
Mbali na Mrisho Bukuku ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kigoma, lakini pia viongozi wengine wa TFF wameambatana na kukagua uwanja huo. Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dr.Harrison Mwakyembe atakuwa mgeni rasmi kwenye mchezo huo.
Ukaguzi huo wa uwanja umekuja ikiwa ni siku moja tu tangu Rais wa FIFA Gianni Infantino aongoze mkutano mkuu wa kikanda wa FIFA uliofanyika jana jijini Dar es salaam huku moja ya masuala yaliyojadiliwa ni maendeleo ya soka la wanawake.
Wakati huohuo Kozi ya makocha wa kozi ya Grassroots kwa watoto wenye umri wa miaka 6-12, Wasichana na Wavulana imeanza Jumatano na inaendelea kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Ujiji,Kigoma.
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done