Friday, 23 February 2018

TASNIA YA UHANDISI UNAKABILILIWA NA UHABA WA WAHANDISI WA KIKE

Na Lucas Myovela

Tanzania bado inakabiliwa na uhaba wa wahandisi wa kike jambo amabalo jambo ambalo linapelekea kukwamisha maendeleo kwa kasi katika kukuza uchumi wa taifa.

Hayo yamesemwa na Kaimu msajili wa bodi ya wahandisi Tanzani Patric Barozi katika semina ya wahandisi kanda ya kaskazini ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wahandisi wa kike huku semina hiyo ikiwahusisha wahandisi kutoka Tanga,Kilimanjaro,Manyara na Arusha.


Patrick ameeleza kuwa hapa nchini bado secta ya sayansi inakabiliwa na uhaba wa wanasayansi ya wa kike ambapo inapelekea uhaba wa waandisi wa kike hapa nchini ambapo kwa kiwango cha wahandii wa kike ni 10 % pekee kulinganisha na wahandisi wa kiume ambao idadi yao ni 90% na kuongeza kuwa nchi ya Tanzania imekuwa ikikuza ustawi wa utoaji wa wanafunzi wengi zaidi ya 60% kulinganisha na nchi za Kenya na Rwanda ambapo ustawi wao ni mdogo huku jumla ya wahandisi wa kanda ya Kaskazini ni 491 na huku walio sajiliwa ni 219 pekee.


Kutokana na changamoto hizo Patric ameeleza kwamba kutokana na sera ya serikali ya awamu ya tano ya tanzania ya viwanda kunauhitaji mkubwa sana wa wahandisi ili taifa kufikia malengo na hivi sasa wameanzisha kampeni ya kuhamasisha wanafunzi waliyopo mashuleni kusoma masomo ya sayansi ili waende katika vyuo vya sayansi na mwishowe waje kuwa wahandisi wazuri kwani taifa bado linahitaji wahandisi  wa kike na wakiume ili kukuza uchumi na kuongeza kuwa mpaka sasa ongezeko la vyuo vya sayansi hapa nchini ni vyuo kumi na moja vinavyotoa taaluma ya uhandisi.


Aidha pia Patrick ametoa rai kwa wanafunzi waliyo maliza masomo yao na kwenda mtaani na kuanza kujiita wahandisi waache mara moja tabia hiyo kwani mwandisi kamili anatakiwa asajiliwe na kupewa reseni ya uhandisi na kuongeza kuwa wazazi bado wanayo nafasi ya kuwashawishi watoto wao kusomea masomo ya sayansi na wao kama bodi kwa kushirikiana na serikali wanahamasisha ujenzi wa maabara hapa nchini ili kuondoa uhaba wa maabara za sayansi.


Awali akifungua semina hiyo mwenyekiti wa kamati ya uendelezaji wahandisi kitaaluma hapa nchini PDAC , Prf Esnat Osinde Chaggu ameemeleza kuwa licha ya waandisi kuwa na mafuaa makubwa katika taifa amewataka wahandisi kutumia fursa za changamoto zilizopo ili kufanikisha miradi mbali mbali na kufikia malengo tarajiwa katika tasnia ya uhandisi na taifa kwa ujumla.


Aidiha  Prf Chaggu aliwataka wahandisi wazoefu katika kazi kuwasaidia kwa ukaribu wahandisi wachanga makazini ili kufanikisha ujenzi wa taifa kwa nyanja zote za kimaendeleo ya sayansi ili kufikia uchumi wa kati wa tanzania ya viwanda na kuwataka wanawake wanaosoma masomo ya sayansi wasikate tamaa katika masomo yao ili kulinisulu taifa kwa uhaba wa wahandisi.


Kufuatia semina hiyo iliyo wahusisha wahandisi kanda ya kaskazini ya kuwajengea uzoefu wahandishi wa kike, Bodi hiyo ya wahandisi inaseherekea miaka 50 tangu kuanzisha kwake na wanategemea kuangalia wapi penye mapungufu ili kuweza kurekebisha na kuweka mikakati madhubuti ya ustawi wa wahandisi katika ngazi za juu.

No comments:

Post a comment