SERIKALI imesema kuwa itaendelea kuhakikisha kuwa inawasaidia na
kuwawezesha wafugaji wa nyuki ili waweze kufuga kisasa na kupata asali
iliyobora ambayo itawasaidia kuwaongezea kipato katika maisha yao.

Naibu waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Mhandisi Stella
Manyanya,aliyasema hayo jana Mkoani hapa alipokuwa akifungua kongamano
la kimataifa la ufugaji wa nyuki linaloendelea mjini hapa.

Alisema kuwa mazao ya nyuki yamekuwa yakichangia shilingi bilioni3.8
katika serikali,hivyo wanatambua umuhimu wa mazao ya nyuki na kwamba
mikakati kabambe inawekwa na serikali kuhakikisha kuwa inawasaidia
wafugaji wa nyuki.

“Wafagaji wanatakiwa kufuga kisasa na kuhakikisha kuwa wanafuga kwa
wingi kwani asali licha ya kuwa ni dawa pia ni rafiki wa mkulima kwani
husaidia kuchavua mazao na pia husaidia katika kumuongezea kipato
mfugaji wa nyuki”alisema naibu Waziri huyo.

Amesema kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na misitu mingi ila inayotumika
kwa ufugaji ni asilimia kumi tu na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza
kwa wingi kuzalisha mazao ya nyuki kwani mazao yake mengi yana faida
lakini watu wengi wamekuwa wakidili na asali n anta pekee.

Kwa upande wake Rais na Afisa Mtendaji mkuu wa Taasisi ya CESO ya
Canada,Wendy Harris,ambao ndio waandaji wa mkutano huo wakishirikiana
na Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo nchini(SIDO),amesema kuwa
kongamano hilo la siku nne linashirikisha nchi 15 kutoka sehemu
mbalimbali ulimwenguni.

Harris alisema kuwa katika kongamano hilo mbinu mbalimbali za ufugaji
wa nyuki kisasa zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na kuangalia masoko ya
uhakika ya mazao ya nyuki  katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa SIDO,Mhandisi Profesa Sylvester
Mpanduji, amesema katika kongamano hilo watajadili kwa kina jinsi gani
wanaongeza uzalishaji wa asli hapa nchini ikiwa ni pamoja na kutumia
mbinu za kisasa katika ufugaji.

“Pia katika kongamano hili wadau wa sekta ya nyuki watajadiliana na
kubadilishana ujuzi na uzoefu wa ufugaji wa nyuki kutoka
kwawawakilishi wan chi mbalimbali wanaoshiriki katika kongamano hilo
Share To:

msumbanews

Post A Comment: