Wednesday, 28 February 2018

RIPOTI: Makanisa 714 yafungwa na serikali nchini Rwanda

Zaidi ya Makanisa 714 nchini Rwanda yamefungwa mjini Kigali kwa kukosa kutimiza vigezo na masharti yaliyowekwa na Serikali ili kulinda usalama wa taifa hilo.
Tokeo la picha la churches in Rwanda
Kwa mujibu wa Gazeti la The New Times zoezi hilo lilianza wiki iliyopita ambapo mpaka kufikia jana zaidi ya makanisa 250 yalikuwa yamefungiwa .
Kwa mujibu wa maelezo ya Afisa wa serikali, Justus Kangwagye kwenye mahojiano na gazeti hilo, amesema makanisa hayo yamekiuka sheria za usalama ikiwepo kukosa viongozi ambao hawana taaluma ya Teolojia.
Kazi ya kuabudu inafaa kufanywa kwa utaratibu na kwa kutimiza masharti ya viwango vya ubora na usalama wa taifa vilivyowekwa. Kutumia uhuru wako wa kuabudu hakuingilii haki za watu wengine. Wametakiwa kusitisha shughuli zote hadi watimize masharti yaliyowekwa,” amesema Justus.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa makanisa mengi nchini Rwanda yanaendesha huduma za kiroho na kuabudu bila vibali maalumu.
Gazeti hilo, limeripoti kuwa watu wengi nchini Rwanda wamepokea taarifa hizo kwa hisia tofauti tofauti wengi wakitaka usajili wa makanisa usihusishwe na masuala ya kisiasa, wengi wakiikosoa serikali kwa uamuzi huo
Tayari Askofu Innocent Nzeyimana wa kanisa Katoliki ambaye pia ni rais wa Baraza la Makanisa katika wilaya ya Nyarugenge ameiomba serikali, kwa niaba ya makanisa, kuyaruhusu makanisa yaliyofungwa yaendelee kuhudumu wakati yakifuatilia usajili.
Chanzo ni kwa mujibu wa gazeti la The New Times.

No comments:

Post a comment