Okwi wa Bukoba ajitokeza kushuhudia Azam FC dhidi ya Kagera Sugar


Kijana mmoja shabiki kindaki ndaki wa mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi amejitokeza kushuhudia mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara baina Azam FC dhidi ya Kagera Sugar uliyopigwa Kaitaba Bukoba.
Kijana huyo aliyejulikana kwa jina la Adam Abubakary kupitia mahojiano na Azam tv, amesema kuwa yeye ni shabiki wa klabu ya Simba na ana mahaba na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi.
“Naitwa Adam Abubakary ni shabiki Simba, nampenda sana Emmanuel Arnold Okwi naishi Bukoba,”ni kauli ya shabiki wa soka Adam Abubakary aliyekuwepo leo kwenye dimba la Kaitaba mjini Bukoba, kushuhudia mechi ya Kagera Sugar na Azam FC.
Anaitwa Adam Abubakary lakini yeye anapenda kujiita ‘Okwi’, ni moja kati ya mashabiki wa soka waliojitokeza na kufuatilia mchezo huo uliyomalizika kwa wenyeji Kagera Sugar kutoka sare ya bao 1 – 1dhidi ya Azam FC.
Mpaka sasa zimebaki mechi mbili pekee kukamilisha duru ya raundi ya 18 ya ligi ambayo imeonekana kutawaliwa na sare huku ikiwa na ukame wa mabao ambapo hadi sasa ni mabao saba pekee ndiyo yaliyofungwa. Mechi zilizosalia ni: Mwadui FC vs Simba SC, Yanga SC vs Majimaji FC.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: