Waziri wa Maliasili na Utalii Dr Hamisi Kigwangalla akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Tanga, ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo la chanzo cha maji ya mto zigi kilichopo ndani ya hifadhi ya mazingira asilia Amani kwa ajili ya kulinda chanzo hicho.
Waziri Kigwangalla ametoa agizo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea eneo la chanzo hicho na kukuta uharibifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya wananchi wanaodaiwa kuchimba madini ya dhahabu katika eneo hilo la hifadhi kinyume cha sheria.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: