Wednesday, 14 February 2018

Hatimaye Rais Jacob Zuma akubali kujiuzulu

Jacob Zuma

Hatimaye rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amekubali kujiuzulu baada ya shinikizo kutoka kwa viongozi wa chama chake cha ANC.
Akizungumza na Waandishi was Habari jana Jumatano Februari 14, 2018 alisema kuwa amechukua maamuzi hayo kwa faida ya taifa lakini hakubaliani na uamuzi wa chama cha ANC.
“ANC haiwezi kugawanyika kwa sababu yangu. Kwa hivyo nimefikia uamuzi wa kujiuzulu kama rais wa nchi mara moja. Licha ya kutokubaliana na uamuzi wa chama changu, siku zote nimekuwa mwanachama mwenye nidhamu wa ANC. 

Nitaendelea kuwatumikia watu wa Afrika Kusini na chama ambacho nimekitumikia maisha yangu yote,”amesema Jacob Zuma.
Awali Chama cha ANC kilimtaka Rais Jacob Zuma aachie madaraka ndani ya Massa 48
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: