Thursday, 22 February 2018

Cannavaro apatwa na msiba wa mwanae


Nahodha wa Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amepatwa na msiba wa kufiwa na mtoto wake anayejulikana kwa jina la Anwar Nadir asubuhi ya leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Hayo yamethibitishwa na taarifa zilizotolewa na uongozi wa timu hiyo na kusema Cannavaro amepokea habari hiyo ya msiba akiwa visiwa vya Shelisheli na wachezaji wenzake.

"Mapema leo asubuhi Canavaro akiwa visiwa vya Ushelisheli amepata msiba wa mwanae Anwar Nadir Ally aliefariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu ya matatizo ya damu. Uongozi wa Yanga SC kwa ujumla chini ya Kaimu Mwenyekiti inatoa pole kwa Nahodha wetu pamoja na familia yake kwa ujumla kwenye kipindi hiki kigumu", imesema taarifa hiyo.

Uongozi wa Msumbanews Media unatoa pole kwa Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' kwa matatizo yaliyomfika pamoja na timu yake kiujumla

No comments:

Post a comment