Articles by "TUZO"
Showing posts with label TUZO. Show all posts

 

Edwin Soko
Maria Sarungi

Kampuni ya SK Media imetoa tuzo haki ya kupata habari na haki ya kujieleza kwa mwaka 2021 / 2022, ambapo Edwin Soko ameibuka kuwa mshindi  wa kwanza wa tuzo hizo.

SK Media wametangaza tuzo hizo kwa kumtangaza Edwin Soko kuwa mshindi wa kwanza kwa kutetea kundi la waandishi wa habari wanaopata madhila  ya kukamtwa na Jeshi la polisi pamoja na mambo mengine yanayowagusa waandishi wa habari.


Mshindi wa pili wa tuzo hizo ni Mwanaharakati Maria Sarungi ambaye amepata tuzo kwa kupaza sauti za wananchi na kuiwezesha jamii kuwasiliana kurahisi kupitia mtandao wa Maria space kupitia mtandao wa twitter.

Mshindi wa tatu, wamegongana Boniface Jacob na Martine Mases ambao walifuatilia kesi ya Freeman Mbowe hatua kwa hatua kwa kutumia simu ya kiganjani.

Washindi hao watapata vyeti na zawadi nyingine mbalimbali.



NA ANDREW CHALE, ZANZIBAR

WASANII muunganiko kutoka nchi Sita, United  Kingdom  (UK), Morocco,  Ghana, Algeria,Tanzania  na visiwani Zanzibar  wamefanya onyesho moja matata lililokonga nyoyo mashabiki wa muziki usiku wa pili wa tamasha la Sauti za Busara Februari 14..

Onyesho hilo la pamoja wasanii hao kwa kila mmoja alionyesha uwezo wa sanaa yake

Kupiga ala za muziki, kuimba na kucheza ambapo kila mmoja aliweza kuonyesha kitu cha tofauti katika  onyesho lao la hilo.

Wasanii Ester  Subi Zawose na Pendo Ukwe Zawose (Tanzania Bara) waliweza kuonyesha ngoma ya Wagogo katika muunganiko wa onyesho hilo.

Msanii Siti Amina (Zanzibar ) nae aliweza kuonyesha uwezo wake jukwaani ikiwemo ule wa kuimba na kucheza.

Munganijo wa vyombo uliojaa ustadi na ubora wa hali ya juu ulitosha kutoa radha halisi ya muziki wa Afrika ambao umekuwa ni wenye kuvutia jamii nyingi.

Wasanii hao pia waliweza kuimba wimbo  'Sawa sawa'  ambao unaendana na ujumbe wa kauli mbiu ya mwaka huu wa tamasha wa kupinga na kukemea unyanyasaji wa kujinsia.
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa Mkoa wa Simiu, Mhe. Anthony Mtaka amepewa tuzo ya elimu ya Tanzania Elimu Awards na Taasisi ya Elimu Solutions, ikiwa ni kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu.

Tuzo hiyo imekabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Solutions, Neithan Swed,  Mjini Bariadi wakati wa uzinduzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu(daraja sifuri) katika mtihani wa Mock kwa lengo la kuwasaidia kuongeza ufaulu wao katika Mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Novemba 2019.

Swed amesema Taasisi hiyo imefuatilia na kuona juhudi zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu katika mapinduzi ya elimu ikiwemo ubunifu wa kuanzisha kambi za kitaaluma ambazo zimeonekana kuwa na mchango mkubwa katika kuongeza ufaulu wa mkoa wa Simiyu kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kutoka mwaka 2016 hadi mwaka 2018.

“Anayoyafanya Mhe. Mtaka hayaishii Simiyu peke yake Tanzania inayaona, tulifuatilia habari za kambi za kitaaluma na tukaangalia nafasi ya mkoa katika matokeo na namna mlivyofanya vizuri, mmeweka alama kwenye Taifa na tunatamani Mhe. Mtaka aziendeleze juhudi hizi zaidi ili mtoke kwenye kumi bora mwende tatu bora na mwakani tupate mwanafunzi bora kutoka Simiyu atakayepata tuzo hii” alisema Neithan Swed.

Katika hatua nyingine Swed amesema Taasisi ya Elimu Solutions itatoa ufadhili kwa mwanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2019 atakayefanya vizuri katika mtihani wa Taifa na kumpeleka nchini China kuendelea na masomo.

Akipokea tuzo hiyo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Taasisi ya Elimu Solutions kwa kutambua juhudi zinazofanywa na mkoa wa Simiyu na kutoa tuzo huku akibainisha kuwa mkoa wa Simiyu unaithamini sana tuzo hiyo.

Aidha, Mtaka ameipongeza Taasisi ya Elimu Solutions namna wanavyohamasisha maendeleo ya Elimu ya Watanzania ikiwa ni pamoja na kutoa ufadhili kwa wanafunzi wanaofanya vizuri kwenda kusoma nje ya nchi.

Tuzo za Elimu Tanzania Elimu Awards zimetolewa na Taasisi ya Elimu Solutions kwa wadau mbalimbali wa elimu waliochangia  na kusaidia kuleta mabadiliko kwa ubunifu na juhudi zao binafsi, taasisi zinazoihudumia sekta ya elimu; pia hutolewa kwa viongozi, walimu, wanafunzi waliofanya vizuri kwenye elimu
Mrembo Sylivia Sebatian Bebwa toka kanda ya ziwa, ameshinda taji la Miss Tanzania kwa mwaka 2019, katika shindano lililofanyika ukumbi wa Kisena  Millennium Tower, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumamosi Agosti 24,2019 .
  
Sylivia anatokea  Jijini Mwanza akiwa ni mshindi wa Miss Mwanza 2019 lakini pia mshindi wa Miss Lake Zone. 

Kutoka na ushindi huo, Silvia ameondoka na kitita cha Sh10 milioni huku mshindi wa pili Grayres Amos akiondoka na sofa yenye thamani ya Sh2 milioni na mshindi wa tatu Qeen Antony akiondoka na Sh1 milioni moja.

HIVI Karibuni Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), lilifanya Maadhimisho ya Miaka 50. Ambapo mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo alikuwa Mh. Majaliwa Kassimu Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye aliwakilishwa na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuuu- Uwekezaji Mhe. Angela Jasmine Kairuki.

Pamoja na Maadhimisho hayo, TPDC ilitoa TUZO kwa baadhi ya WASTAAFU waliokuwa na michango mbalimbali katika utumishi wao. Pichani juu Bi Marie Msellemu, MKUU wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa TPDC, akimkabidhi Prof. Mark Mwandosya TUZO ya kuutambua mchango wake mkubwa kwa TPDC kwa nafasi yake kama Kamishna wa kwanza wa Petroli nchini na Mwenyekiti wa BODI ya Shirika la TPDC katika utumishi wake.
Picha ya pamoja.
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza na watumishi wa mamlaka hiyo mara baada ya kufanikiwa kupata tuzo hiyo kulia ni
 Afisa Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Haika Ndalama akizungumza wakati wa halfa hiyo
Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Dorrah Killo  akizungumza wakati wa halfa hiyo

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akiwa amebebwa na watumishi wa mamlaka hiyo wakimpongeza baada ya kupata tuzo hiyo
 Watumishi wa mamlaka hiyo wakiwa na tuzo hiyo
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kushoto ambaye amevaa koti akiwa na watumishi wa mamlaka hiyo wakisheherekea ushindi wa tuzo hiyo
 Watumishi wa Mamlaka hiyo wakicheza kwa furaha baada ya kupata tuzo hiyo
 Watumishi wa mamlaka hiyo wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye halfa hiyo
 Watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye halfa hiyo
 Msafara wa magari na pikikpiki ukitokea eneo la Pongwe Jijini Tanga wakielekea Ofisi za Mamlaka ya Maji Jijini Tanga mara baada ya mapokezi ya tuzo hizo



MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imepata tuzo kwa kuwa mamlaka bora katika utoaji wa huduma za maji safi kwa mamlaka za mikoa 25 Tanzania kwa mwaka 2017/2018.

Tuzo hiyo ilitolewa na Mamlaka ya Udhibiti Nishati na Maji nchini (EWURA) kutokana na utendaji kazi wao na utoaji wa huduma baada ya kufanya tathimini na hivyo kujikuta wakifanikiwa kuigia kwenye nafasi hiyo ya kuny’akua tuzo hiyo.

Akizungumzia namna walivyopokea tuzo hiyo baada ya mapokezi makubwa yaliyoanzia eneo la Pongwe Jijini Tanga Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly alisema wanafurahi kutokea tuzo hiyo kmuwa mamlaka bora katika huduma ya maji safi kati ya mamlaka 25 Tanzania bara ni faraja kubwa sana kwao.

Alisema wameipata tuzo hiyo kwa sababu wamekuwa na nia ya kuipata kutokana na ufanisi mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii kwa maarifa huku wakijua vigezo vinavyotakiwa na vigezo kwa ujumla wake ni ubora wa huduma kwa wananchi wanapata maji muda wa kutosha na maji bora.

Alisema pia ni kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama maji kwa kuwafikia watu wengi iwezekanovyo huku wakipunguza upotevu wa maji ambayo vimechangia wao kuonekana mamlaka bora ya kwanza Tanzania bara kutoa huduma ya maji safi 2017/2018,

Mkurugenzi huyo alisema baada ya kupata tuzo hiyo hivi sasa mikakati yao ni kuendelea kujipanga kutambua jinsi vigezo vinafanyiwa kazi ili kupata mamlaka bora kila mwaka kutokana na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

“Tumejipanga na Tutatekeleza yale yanafanyika kwenye vile vigezo tuendelee kubaki kuwa mamlaka bora Tanzania bara na ulimwengu mzima kama ilivyo malengo yetu “Alisema Mkurugenzi huyo.

Awali akizungumza katika halfa hiyo Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Dorrah Killo alisema baada ya kupata tuzo hiyo wataendelea kupambana kuhakikisha wanaendelea kung’ara katika utoaji wa huduma hapa nchini

“Tukienda mwakani vigezo zinaweza kuwa vikubwa hivyo tutaendelea kujipanga lakini niwaambie kwamba tumewatupa mbali sana wenzetu waliokuwa karibu nasi..hii inatokana na jitihada kubwa za bodi ya wakurugenzi,uongozi na wateja wao”Alisema Afisa Uhusiano huyo.

Alisema suala linguine ni kuwahudumia wateja wao vizuri kwani bila kuwahudumia wateja na kutoa elimu nzuri kwao wasingeweza kufikia hatua hiyo wanashaukru wateja wao na wafanya kazi kwa bidii washirikiana wapendani ili kufikia malengo yao.

Mwisho.