Articles by "MAFUNZO"
‏إظهار الرسائل ذات التسميات MAFUNZO. إظهار كافة الرسائل

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), wameendesha mafunzo kwa viongozi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa kutoka mikoa  ya Kilimanjaro, Manyara, Dodoma, Mara,  Kigoma, Shianyanga,Mbeya, Morogoro, Dar es salaam, Lindi, Mtwara na Pwani  juu ya  ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi. 

Viongozi hao wa Vituo vya Taarifa na Maarifa, wamejifunza umuhimu wa ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi hasa katika uchaguzi wa serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba 2024, na kupoitishwa kwenye ratiba ya matukiko ya uchaguzi ilki waweze kushiriki kila hatua ikiwa ni pamoja na kuwasisistiza wanawake kujitokeza na kushiriki kikamilifu. 

Mwezeshaji wa Mafunzo Deo Temba akiwasilisha mada kuhusu dhana za jinsia na ushiriki wa Wanawake katika uongozi wakati wa warsha ya mafunzo kwa washiriki kutoka vituo vya Taarifa na Maarifa yakiwa na lengo la  kuongeza uelewa kwa washiriki ili ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi na ngazi za maamuzi kuongezeka, kuwajengea uelewa wa pamoja kuhusu mifumo ya uchaguzi wa serikali za mitaa na fursa zilizopo katika kuwezesha wanawake kushiriki nafasi za maamuzi yaliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki kutoka vituo vya Taarifa na Maarifa wakichangia mada kwenye mafunzo ya kuwaongezaa ujuzi kuhusu ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi na ngazi za maamuzi kuongezeka pamoja na kuwajengea uelewa wa pamoja kuhusu mifumo ya uchaguzi wa serikali za mitaa na fursa hasa kwa uchanguzi wa mwaka 2024 kwenye mafunzo hayo yanayofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mtandano wa Jinsia Tananzaia (TGNP) pamoja na washiriki kutoka Vituo vya Taarifa na Maarifa pamoja wakifuatilia mada kutoka kwa wataalam wa TGNP kwenye mafunzo ya siku tatu yanayofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.


Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umefanya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji  kutoka katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF), ACT Wazalendo, Chama cha Kijamii (CCK) na NCCR Mageuzi ili kutambua masual,a muhimu ya kijinsia katika uongozi. 

Mafunzo hayo ni sehemu ya shughuli za TGNP za kila mwaka za kujenga uwezo kwa viongozi wanawake ili kutambua umuhimu wa kuzingatia masuala ya kijinsia katika kutekeleza afua mbalimbali ikiwepo uandaaji wa mipango, miradi ya maendeleo inaytozingatia mahitaji ya kijinsia kwa makundi yote. 

Wanawake wanaoshiriki mafunzo haya wanatoka katika kata na halmashauri tofauti ambao wapo kwenye program maalum ya malezi (ukungwi) na ushauri (Mentorship and Coaching) inayolenga kuwajenga  kuwa viongozi bora ikiwepo kuwajengea uwezo na ujasiri wa kusimama mbele za watu na kujieleza, ikiwa ni pamoja na kuvunja vikwazo vinavyosababisha ukatili wa kijinsia na  kukwamisha ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi na maamuzi. 

Akizungumza kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP,  Mkuu wa Program Mafunzo ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Anna Sangai, amesema lengo kuu la warsha hiyo ili kuongeza uelewa wa dhana ya jinsia na uongozi pamoja na kujenga uelewa wa pamoja kuhusu mifumo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na fursa zilizopo katika kuwezesha wanawake wanashiriki kwenye nafasi za maamuzi.

Pia amesema wanaweka mikakati ya pamoja ya kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi kwenye kata, vijiji, mitaa na vitongoji husika pamoja na kuimarisha mahusiano na kujenga nguvu ya pamoja na kayoka kutekeleza ajenda ya usawa wa kijinsia katika siasa.

Aidha, Anna amesisitiza kwamba, licha ya nafasi za kisiasa zinazogombewa katika uchaguzi wa serikali za Mitaa, pia zipo fursa nyingine za uongozi ambazo wanawake wanaweza kuzishika zikiwepo Kamati, Bodi za afya, elimu, AMCOS na mabaraza ya ardhi ambako ni maeneo muhimu kwa maendeleo yanayohitaji ushiriki wa wanawake.
Afisa wa Program Mafunzo wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Anna Sangai akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji wa Mafunzo Deo Temba akiwasilisha mada kuhusu dhana za jinsia na ushiriki wa Wanawake katika uongozi kwa washiriki kutoka vyama vya siasa mbalimbali katika warsha ya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakichangia mada kwenye warsha ya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF), ACT Wazalendo, Chama cha Kijamii (CCK) na NCCR Mageuzi wakifuatilia ufunguzi pamoja na mada zilizokuwa zinatolewa wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.


MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba kulia  akikagua gwaride la vijana wahitimu wa mafunzo kwa mujibu wa sheria Operesheni Jenerali Venance Mabeyo kikosi cha 835 KJ cha Mgambo JKT wilayani  Handeni  Mkoani Tanga
 Gwaride la vijana wahitimu wa mafunzo kwa mujibu wa sheria Operesheni Jenerali Venance Mabeyo kikosi cha 835 KJ cha Mgambo JKT wilayani  Handeni  Mkoani Tanga wakipita mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo
 gwaride la vijana wahitimu wa mafunzo  kwa mujibu wa sheria Operesheni Jenerali Venance Mabeyo kikosi cha 835 KJ cha Mgambo JKT wilayani  Handeni  Mkoani Tanga wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo 

Na Oscar Assenga HANDENI.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amewataka vijana waliohitimu wa mafunzo ya Operesheni Mabeyo 2022 wanakwenda kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini kuhakikisha wanatumia vizuri mitandao ya kijamii kwa faida badala ya kuhakikisha wanajiepusha na matumizi mabaya.
na sio vyenginevyo

RC Mgumba aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya katika kambi ya JKT Kabuku 835 KJ wilayani Handeni wa mujibu wa Sheria Operesheni Jenerali Venance Mabeyo 2022,ambapo alisema kwa sababu vijana wengine waliopo vyuoni wamekuwa na uhuru uliopitiliza na kufanya mambo bila uwepo wa usimamizi.

Alisema lazima wazazi washirikiane katika kuwatembelea watoto wao mara kwa mara kwa maana unaweza kujua mtoto wao anasoma kumbe anasomeshwa jambo ambalo baadae linaweza kuwa na athari kwake na Jamii kwa ujumla.

"Niwasihi wazazi wenzangu muwe mnafanya kuwatembelea watoto wenu wanapokuwa vyuoni lakini wahitumu leo niwaase mkatumie vizuri mitandao ya kijamii kwa ajili ya faida na sio nyenginevyo maana vijana wengine waliopo vyuoni anaweza kudanganywa mwenye mitandao ya kijamii ukashurutishwa jambo ambalo unaweza kufanya kwa tamaa"Alisema

Mkuu huyo wa Mkoa alisema matokeo yake wanadhalilisha wazee wao Jamii na Ndugu na Taifa kwa ujumla hivyo hakikisheni suala la nidhamu wanalishikilia kweli hasa wale wanaoenda kuishi vyuoni.

"Kwa sababu mtakumbana na watu mbalimbali ikiwemo wanasheria wasije kuwapotosha nyie mmeiva na mmefundwa nidhami na uadilifu kaishini maisha hayo"Alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Awali akizungumza wakati wa ufunguji wa mafunzo hayo Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele aliwataka wahitimu wa mafunzo wasiende kutu mika vibaya katika maeneo mrakayokuwepo wakati wote mkumbuke kiapo mlichoapa.

Alisema kuwa kama wanavyofahamu majukumu ya JKT ni malezi ya vijana na uzalishaji wa mali na kufanya shughuli za ulinzi wa Taifa katika kutekeleza majukumu hayo ya kila siku.

Hata hivyo alisema hivyo kutolewa mafunzo hayo kwa vijana wa mujibu wa sheria na mafunzo ya mujibu wa sheria op Jenarali Mabeyo yamekuchukua muda wa majuma 12 mfululizo.

Mkuu wa Jkt alisema kwamba wahitimu hao wamejifunzamasomo mbalimbi yakiwemo ya uzalishaji mali,nadharia na vitendo kwa ujumla lengo kukuza moyo wa uzalendo kuwajengea nidhamu ,ukakamavu na ujasiri.

Alisema hiyo itawafanya wajitambue kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuilinda,kuijenga na kuitetea nchi yao.

Naye kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha 835 KJ JKT Kabuku Luteni Kanali Raymond Mwanri alisema vijana hao wakiwa kwenye mafunzo hayo wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo ulinzi wa Taifa lao,Uzalendo na utii kwa mamlaka zilizowekwa kwa mujibu wa sheria 

Hata hivyo aliwataka wahitimu hao kuhakikisha wanakiishi kiapo hicho huku akieleza wamefaulu katika viwango mbalimbali vya kuhitimua mafunzo hayo.

Hata hivyo kwa upande Mkuu wa Mafunzo wa JKT Tanzania Kanali Aisha Matanza alisema mafunzo ya vijana ya kujitolea kwa mujibu wa sheria ya Jenero Mabeyo yamekuwa chachu kuweza kuwaimarisha vijana kuwafanya wakakamavu na wazalendo kwa nchi yao.

Ofisa Mfawidhi wa Shirika hilo Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akitoa elimu kwa wavuvi, wamiliki wa vyombo wa Vijiji vya Petukiza na Moa wilayani Mkinga kuhusu usalama na umuhimu wa kuwa na vifaa vya kujiokolea ikiwemo maboya wakati wanapokuwa wakifanya shughuli zao za majini kila siku.
Ofisa Mfawidhi wa Shirika hilo Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akitoa elimu kwa wavuvi, wamiliki wa vyombo wa Vijiji vya Petukiza na Moa wilayani Mkinga kuhusu usalama na umuhimu wa kuwa na vifaa vya kujiokolea ikiwemo maboya wakati wanapokuwa wakifanya shughuli zao za majini kila siku.
Ofisa Mfawidhi wa Shirika hilo Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua akiwaonyesha wavuvi kifaa cha kuzimia moto ambacho ni muhimu viwepo kwenye vyombo vyao
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kijiji cha Petukiza Kata Moa wilayani Mkinga Mrashi Kea Kasim akizungumza kushoto ni Ofisa Mfawidhi wa Shriika la Tasac Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua
AFISA Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la TASAC Kitengo cha Mahusiano na Masoko Amina  Miruko akieleza jambo wakati wa utoaji wa elimu hiyo
OFISA Mfawidhi wa TASAC Mkoa wa Tanga Captain Christopher Shalua kushoto akiwaonyesha wavuvi namna ya kuweza kuvaa moja ya  vifaa vya kujikolea wanapokuwa wakiingia majini kufanya shughuli zao za kila siku
OFISA Mfawidhi wa TASAC Mkoa wa Tanga Captain Christopher Shalua kushoto akisisitiza jambo kulia ni AFISA Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la TASAC Kitengo cha Mahusiano na Masoko Amina  Miruko


NA OSCAR ASSENGA, MKINGA.

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoa wa Tanga limekutana na wavuvi, wamiliki wa vyombo wa Vijiji vya Petukiza na Moa wilayani Mkinga kwa ajili ya kutoa elimu ya usalama wa vyombo vya majini na umuhimu wa kuwa na vifaa vya kujiokolea ikiwemo maboya wakati wanapokuwa wakifanya shughuli zao za majini kila siku.

Akizungumza wakati akitoa elimu hiyo,Ofisa Mfawidhi wa Shirika hilo Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua alisema vyombo vidogo vya majini vinapaswa kuzingatia usalama na utunzaji wa mazingira ikiwemo matumizi sahihi ya maboya ya kujiokolea.

Alisema pia ni muhimu wakatambua matumizi sahihi wakati wa kuyavaa kutokana na muhimu kuyavaa muda wote wanapokuwa kwenye shughuli za uvuvi au kusafiri majini ili kuweza kuwasaidia pindi wanapokumbana na majanga mbalimbali.

Captain Shalua alisema walikuwa wakiwaelimisha wavuvi ili waweze kupata uelewa juu ya matumizi sahihi ya vifaa ambavyo kwa mujibu wa sheria vinapaswa kuwepo kwenye vyombo.

“Lakini pia vifaa vyengine ambavyo vinapaswa kuwepo kwenye vyombo vyenu ni vya kuzimia moto na vile kwa ajili ya huduma ya kwanza kwani vina umuhimu wakati wa dharura ni wakati gani mvuvi anaweza kuvitumia ili viwe msaada kwake”Alisema Captain Shalua.

Hata hivyo alisema kwa mfano vyombo vingi vya uvuvi vinatumia mafuta ya petrol kwa ajili ya kuendesha mashine zao kwa hiyo moto unapowaka kutokana na mafuta hayo hawawezi kuzima kwa kutumia maji badala yake wanaweza kuuzima kwa kutumia mchanga au poda maalumu iliyopo kwenye mitungi.

Aliongeza kwamba pia wanaweza kutumia mapovu maalumu yaliyopo kwenye mitungi hivyo elimu yao ilijikita kwenye maeneo hayo ili iweze kuwasaidia wavuvi wanapokuwa mbali na nchi kazi wanapopata majanga ya waweze kujisaidia na kuokoa mali na kuwaepusha na kupoteza maisha.

Awali akizungumza wakati wa mkutano huo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kijiji cha Petukiza Kata Moa wilayani Mkinga Mrashi Kea Kasim alisema wavuvi wamesikiliza elimu hiyo na changamoto kubwa wavuvi wamekuwa wamekufa baharini kutokana na kuwa na vifaa vya kujiokolea.

“Tunaiomba Serikali ione namna ya kutusaidia wavuvi nasi baadae tuweze kununua kwani ni ukweli kwamba wavuvi wanapotoka nchi kavu kwenda baharini kuna urefu mkubwa na mtu anaachwa mita 20 pekee yake bila msaada na wakati mwengine kujiokoa anapopata dhoruba inakuwa ni mgumu”Alisema

Alisema kutokana na kwamba Serikali inaingiza mapato makubwa sana kutokana na ukusanyaji wa maduhuli hivyo wanaiomba iwaangalie kwa unyonge kwa kuwawezesha ili baadae waweze kujinunulia wenyewe vifaa vya usalama.

Naye kwa upande wake Mkazi wa Kijiji cha Petukiza Kasim Ally alisema kwamba elimu hiyo itakwenda kuwasaidia wakati wakitekeleza shughuli zao mbalimbali za uvuvi .

“Kwanza nilishukuru shirika la Tasac kwa kuona umuhimu wa kuja kutupa sisi wavuvi elimu na tunahaidi tutakwenda kuifanyia kazi kwa mapana makubwa “Alisema Kasim.

Mwisho.

Afisa Elimu Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Mkoa wa Tanga Salim Bakar akizungumza wakati akifungua mafunzo  maalumu kwa wafanyabiashara Jijini Tanga waliosajiliwa na kodi ya ongezeko la Thamani (VAT).
Afisa Elimu Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Mkoa wa Tanga Salim Bakar akizungumza wakati akifungua mafunzo  maalumu kwa wafanyabiashara Jijini Tanga waliosajiliwa na kodi ya ongezeko la Thamani (VAT).

MMOJA wa wafanyabiashara walioshiriki mafunzo hayo akizungumza na waandishi wa habari ambapo alipongeza mfumo huo mpy

Sehemu ya wafanyabiashara wakifuatilia mafunzo hayo
Sehemu ya wafanyabiashara wakifuatilia mafunzo hayo



NA OSCAR ASSENGA, TANGA

 MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga wametoa mafunzo maalumu kwa wafanyabiashara Jijini waliosajiliwa na kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuhusu mfumo mpya ulioboreshwa wa uwasilishaji wa Ritani ya Kodi la Ongezeko la Thamani (VAT).

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Afisa Elimu Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Mkoa wa Tanga Salim Bakar wakati wa mafunzo maalumu kwa wafanyabiashara Jijini Tanga waliosajiliwa na kodi ya ongezeko la Thamani (VAT). 

Alisema mafunzo hayo yanakuwa endelevu kwa wilaya nyengine kuhusiana mfumo mpya ulioboreshwa wa uwasilishaji wa ritani za kodi la ongezeko la thamani (VAT) kwa walipa kodi pindi yanapojitokeza mabadiliko, marekebisho ya sheria za kodi lengo ni kukuza uelewa wa wafanyabiashara wanapotumia mifumo kuwasilisha ritanio za kodi.

 Alisema mamlaka hiyo imeanzisha mfumo wa uwasilishaji wa Ritani ulioboreshwa na ilitoa Taarifa mwezi February mwaka huu na kwamba kuanzia ritani za mwezi Machi za VAT ambazo zinawasilishwa mwezi Aprili walipa kodi watapaswa kutumia mfumo mpya ulioboreshwa wa uwasilishaji wa ritani.

 Afisa huyo alisema mfumo huo utakuwa na faida nyingi ikiwemo urahisi kwa mtumiaji ambapo mlipakodi atahitajika kutumia akaunti moja ya uwasilishaji wa ritani tofauti na awali ilikuwa ikimlazimu mlipakodi kutumia tofauti kulingana na aina ya ritani ya kodi.

 Aidha alisema faida nyengine ni ujazaji wa ritani umerahisishwa ambapo taarifa za manunuzu katika ritani ya VAT zitaingizwa kwa kutumia namba ya uthibitisho (Verfication Code) tu iliyopo katika risiti ya kieletroniki tofauti na awali ambapo itamlazimu mlipakodi kujaza taarifa za kadhaa kama Jina la Muuzaji, Namba ya Usajili wa VAT, Namba na tarehe risiti/ankra, Kiasi cha Manunuzi na VAT katika manunuzi husika.

 “Kwa kweli mfumo huo mpya utaongeza mapato ya serikali na lengo la serikali ni kumrahisishia mlipakodi atape huduma iliyoboreshwa bila kufika TRA na hivyo atapata kuwasilisha ritani akiwa ofisini au nyumbani bila kufika TRA”Alisema

Hata hivyo alisema mfumo huo utawezesha kufanyika kwa marekebisho ya kodi pale yanapotokea kama yalivyoanishwa katika sheria ya kodi la ongezeko la thamani sura ya 148 tofauti na utaratibu wa sasa ambapo mlipakodi alihitajika kuandika barua ya kutoa taarifa kwa Kamisha. 

Awali akizungumza mmoja wa wafanyabiashara hao kutoka SD Supermarket Moniraju Vasant alisema wanashukuru kupatiwa elimu hiyo ya mabadiliko hayo na kwamba mpango huo utakuwa ni mzuri kwa ajili ya kuboresha mapato TRA. 

Alisema pia utawapunguzia usumbufu wa kwenda TRA kupata huduma badala yake kutumia mifumo hiyo wakiwa ofisini kwao na hivyo kuwawezesha kutekeleza majukumu mengine