
Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi, akifungua semina ya mafunzo kwa waajiri kutoka Taasisi na Halmashauri za Mkoa wa Dodoma kuhusu majukumu na Huduma zitolewazo na PSSSF
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifiatilia hotuba na mawasilisho mbalimbali ya mada
Dodoma, Oktoba 6, 2026
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umeahidi kulinda haki na maslahi ya wanachama wake, kurahisisha huduma na kudumisha mahusiano na mawasiliano ya wazi na Waajiri kote nchini.
Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Paul Kijazi wakati akifungua semina iliyohudhuriwa na waajiri 462 wa kanda ya kati iliyofanyika Oktoba 6, 2026, Makao Makuu ya PSSSF jijini Dodoma.
Semina hiyo ililenga kujenga uelewa wa pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Mfuko na Waajiri ili kurahisisha utatuzi wa changamoto za wanachama na kuboresha utoaji wa huduma.
Semina hiyo iliyohudhuriwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Hajji Khamis na Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw. Sayi Lulyalya, Bw.Kijazi alisisitiza umuhimu wa Waajiri kutimiza wajibu wao kwa wakati na kutumia mifumo ya kidigitali ili kulinda haki na maslahi ya watumishi kwa lengo la kuharakisha huduma.
“Hatua za kuimarisha mifumo ya kidigitali na ushirikiano wa karibu zinatarajiwa kuondoa ucheleweshaji wa malipo ya mafao, kuhakikisha taarifa za wanachama zinahuishwa mara kwa mara, na kuongeza ufanisi wa jumla katika utoaji wa huduma zetu” alifafanua Bw. Kijazi
Katika semina hiyo, mada mbalimbali ziliwasilishwa na kujadiliwa ikiwemo; matumizi ya Mfumo wa PSSSF Member Portal, Uwasilishaji wa Nyaraka za Madai ya Mafao, na Taratibu za Usajili wa Watumishi wapya.</






Post A Comment: