-Ziara ya kikazi ya kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu bora za kuwahudumia wateja

Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Uhusiano wa Umma na Mawasiliano cha Shirika la Posta Tanzania (TPC) kimetembelea Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu bora za kuboresha huduma kwa wateja.

Ziara hiyo iliongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Uhusiano wa Umma na Mawasiliano wa TPC, Bi. Jamila Mbarouk, akiambatana na Bi. Jane Salu pamoja na watumishi wengine wa kitengo hicho. Katika ziara hiyo, timu hizo zilibadilishana mawazo kuhusu namna ya kuwahudumia wateja kwa ufanisi, kushughulikia changamoto zao na kuhakikisha wanapata huduma zinazokidhi mahitaji yao.

Kwa upande wa TANESCO, timu iliongozwa na Meneja Msaidizi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Bw. Shamu Lameck Ruyebo, akiambatana na Bw. Fadhil Msuya na Bi. Janeth Bannali. Ziara hiyo ilitoa fursa kwa timu hizo kujifunza kutokana na uzoefu wa kila upande na kujadili namna ya kuendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Posta Tanzania za kuimarisha huduma kwa wateja kupitia kujifunza na kubadilishana uzoefu na taasisi nyingine. Kupitia hatua hiyo, Shirika linalenga kuongeza ufanisi wa watumishi, kuboresha uzoefu wa wateja na kuimarisha kuridhika kwao na huduma zinazotolewa.
Share To:

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: