KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Abdalla Hamid, amesema Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anataka viongozi wote kuwajibika kikamilifu katika kuwahudumia wananchi na kutatua changamoto zinazowakabili.
Rabia ameyasema hayo leo, Septemba 23, 2026, wakati akiendelea na ziara ya CCM katika Mkoa wa Dodoma yenye lengo la kusikiliza, kuzungumza na kutatua changamoto za wananchi kutoka makundi mbalimbali ya kijamii.
Katika ziara hiyo, Rabia amekutana na wananchi waliojitokeza kuwasilisha changamoto, maoni, ushauri na mapendekezo mbalimbali yanayohusu maisha na maendeleo yao.
Baada ya wananchi kuwasilisha changamoto zao, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amejibu hoja zilizowasilishwa na kuahidi kuendelea kuwahudumia wananchi wa mkoa huo kwa ufanisi.
Aidha, Rabia amesema viongozi wanapaswa kuwa karibu na wananchi, kuwasikiliza na kuhakikisha changamoto zao zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati, akisisitiza kuwa huo ndiyo mwelekeo unaotolewa na uongozi wa juu wa CCM na Serikali.
Katika hatua nyingine, Rabia amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kazi nzuri anayofanya katika kuwahudumia wananchi pamoja na kuwa msikivu kwa changamoto zao.














Post A Comment: