Na Denis Chambi Tanga.


WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso  amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa tanki la Maji  lenye wezo wa kuhifadhi maji Lita Milion 60 katika chanzo cha Maji kilichopo Mowe chini ya Mamlaka ya Maji Tanga Uwasa kuhakikisha kuwa anaukamilisha kwa wakati huku akisisitiza kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza kulingana na Mkataba.

Waziri Aweso ametoa maagizo hayo leo wakati alipotembelea mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya  China Railway Seventh Group Limited (CRSG) ambapo amemtaka Mkandarasi kuongeza kasi ya utendaji kazi uli uweze kukuamilika November 30, 2026 na hatimaye kutimiza adhima ya serikali katika kuboresha huduma ya Maji kwa wananchi wa Wilaya za Tanga, Muheza na Mkinga.

"Hatutakuwa na muda wa nyongeza utendaji kazi wa mradi huu uanze kubadilika kuanzia sasa kwa sababu fedha zake zipo ni suala la Mkandarasi kuongeza nguvu kazi na muda pia ubadilike afanya kazi usiku na mchana kabla ya mwezi November tutakuja Tena kuona maendeleo ya mradi" amesema Aweso.

Aidha Aweso ameongeza kuwa baada ya kukamilisha mradi huo Wizara inatarajia kuanzisha mradi mwingine wa hati fungani ambayo itafadhiliwa na mfuko wa maji kwa lengo la kuendelea kuboresha utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi hapa nchini.

Awali akizungumza Mkurugenzi  wa Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Mhandisi Geoffrey Hilly amesema kuwa mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 72 ambapo utakapokamilika wananchi wataweza kupata huduma ya maji safi na salama kwa  saa 18 kwa siku.

Amesema lengo lao ni kuhakikisha wanaboresha utoaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa wilaya za Tanga , Muheza na Mkinga huku akiahidi kulisimamia agizo la Waziri la kumsiamia Mkandarasi juu ya utekelezaji wa miradi huo.

"Mradi huu unaotekelezwa kwa hati fungani mpaka kufikia sasa unaendelea vizuri  ukifikia wastani wa asilimia 72 kwa ujumla wake kuanzia kwenye chanzo na kule mtaani ambako tunasambaza Bomba kwa wananchi utanuzi wa mtambo ni kutoka lita za ujazo 45 mpaka lita 60 ili kuweza kuzalisha maji kwa wingi  kulingana na uhitaji uliopo" amesema.

Ameongeza kuwa jumla mita 10,000 za malipo ya kabla zinatarajiwa kufungwa kwa  hii ikilenga kuondoa malalamiko ya baadhi ya wananchi wakati wanapopelekewa Bili zao za matumizi ya maji Kila baada ya mwezi wakidai kuwa ni kubwa kulingana na kiwango cha maji aalichotumia.

"Mradi huu pia una mita za malipo kabla elfu kumi ambazo zitasaidia kuondokana na migogoro ya wananchi kuhusu bili za Kila mwezi wengine wanalalamika kwamba zile bili hawazielewi kwahiyo mtu atakuwa analipiza maji kadiri anavyotumia." Amesema Mhandisi Hilly.

Kwa upande wake Mkandarasi anayetekeleza mradi huo kutoka Kampuni ya  China railway seventh Group, Dai Bin amesema  kuwa wamepokea maelekezo Waziri wa maji Jumaa Aweso kuhusu utendaji kazi na akiahidi kukamilisha mradi huo kuendana na Mkataba.

Mradi huo ambao inatekeleza kwa fedha za hatifungani kiasi cha Shilingi Bilioni 53.12 zikihusisha utunzaji wa vyanzo mbalimbali vya maji kukarabati wa miundombinu ya majitaka pamoja na uendelezaji wa miradi ya majitaka  ndani ya jiji la Tanga.





Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: