Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Moshi Vijijini umewaalika vijana na wananchi wote kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani yatakayofanyika Agosti 12, 2026, katika Viwanja vya UVCCM Himo, kuanzia saa 4:00 kamili asubuhi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Moshi Vijijini, Yuvenali Ole Rafaeli Shirima, amesema maadhimisho hayo yanalenga kuwaunganisha vijana, kuimarisha mshikamano, uzalendo na kuwahamasisha kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Taifa.
Amesema maadhimisho hayo yatawakutanisha vijana kutoka maeneo mbalimbali pamoja na viongozi wa Serikali, Chama, taasisi na wadau wa maendeleo kwa ajili ya kujadili nafasi ya vijana katika ujenzi wa Taifa na kuhamasisha matumizi ya fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Shirima ametoa wito kwa vijana wa Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoa wa Kilimanjaro na maeneo mengine kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maadhimisho hayo, akisisitiza kuwa vijana ni nguvu muhimu katika kulinda amani na kuharakisha maendeleo ya nchi.
Maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika chini ya kaulimbiu isemayo:
“Vijana ni Nguvu ya Taifa; Tushirikiane Kulinda Amani kwa Maendeleo ya Taifa Letu.”
#SikuYaVijanaDuniani2026 #UVCCMMoshiVijijini #VijanaNiNguvuYaTaifa #Kilimanjaro

Post A Comment: