Zaidi ya wananchi 5,000 kutoka vijiji vitatu vya kata ya Endamaghaay, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, wameanza kunufaika na mradi wa maji safi na salama ulitekelezwa na wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) uliolenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilion 1.9.

Mradi huo umewekwa jiwe la msingi na Kiongozi wa Mabio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 Wazo Michael Mwang’onda na ameridhishwa na utekelezaji wa Mradi huo unaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za maji na kupunguza adha ya kubeba maji umbali mrefu

Akitoa taarifa ya mradi huo, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara mhandisi James Kionaomela, amesema mradi huo unahusisha tanki la kuhifadhi maji lenye uwezo wa kubeba lita 100,000 na utawawezesha wananchi kuunganishiwa huduma ya maji moja kwa moja majumbani, hatua itakayorahisisha upatikanaji wa maji kwa jamii.

Aidha, baadhi ya wananchi walionufaika na mradi huo wameishukuru Serikali kwa utekelezaji wake, wakisema utapunguza umbali wa kufuata maji, kuokoa muda Pamoja na kuongeza fursa za kufanya shughuli za maendeleo.
Share To:

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: