Na.Ashura Mohamed-Arusha
Maonesho ya Sanaa ya Kazi za Ufundi,Uchoraji na Uchongaji yanatarajia kukutanisha zaidi ya wasanii 1500 duniani lengo likiwa ni kutangaza na kukuza saana ya Ufundi nchini ikiwa ni pamoja na kuwafungulia Masoko ya kimataifa wasanii hao.
Akizungumza Jijini Arusha na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maonesho hayo,Makurugenzi mwenza wa Tanzania International Tourism Festival bwana Ibrahim Jama amesema wanalenga kutangaza utalii na utamaduni pamoja na vivutio vilivyo ndani ya nchi ya Tanzania.
"Katika kudumisha utalii,sanaa na utamaduni Wetu ni maonyesho haya yatakuwa yenye vivutio vya sanaa ya uchongaji na pia kutakuwa na warsha ya kuelekeza kuhusu sanaa nzima ya uchongaji yenye maelekezo ya elimu na Maendeleo na kulinda sanaa ya uchongaji."Alisisitiza Ibrahim
Pia amesema kuwa wasanii hao watapata fursa ya kupata ya kupata elimu kuhusu sanaa nzima mwenendo halisi wa soko la sanaa ndani ya nchi katika uchongaji na uchoraji na michezo kujua wajibu wao katika kuingiza kipato kikubwa haswa fedha za. kigeni.
Aidha Wadau ambao watashiriki mkutano huo watapata fursa ya kutembelea vivutio vilivyopo katika Mkoa wa Arusha ili kuendelea kuiunga Mkono serikali katika kuendeleza utalii wa ndani pamoja na maonyesho ya bidhaa za Uchoraji na Uchongaji yatakayofanyika kwa siku tatu.
Bi Rukia Walele ni Raisi wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA ) amesema kuwa Shirikisho hilo linaundwa na wachoraji,wachongaji,wasusi,wanaofuma vitambaa,Wanamitindo na wabunifu wa Mavazi na Viatu ambapo lengo ni kutoa elimu Maalum ya sekta ya Utalii ili kutumia majukwaa hayo kupata elimu zaidi na ushiriki wa kundi hilo bado sio wa kuridhisha.
Kupitia maonyesho hayo watawezeshwa kuingia katika mfumo rasmi wa kupata kipato na kupata Maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na kuliingizia Taifa fedha za kigeni.





Post A Comment: