Siku hiyo ilikuwa ya kawaida kama nyingine. Niliamka mapema, nikamvalisha mwanangu mdogo Brian mavazi safi, na tukaelekea sokoni Kariakoo kufanya manunuzi. Alikuwa na miaka minne tu, mwenye tabasamu tamu na mcheshi kiasi kwamba hata wafanyabiashara walimzoea.

Nikiwa kwenye kibanda cha mbogamboga, nilimwacha pembeni kidogo tu, macho yangu yakiwa kwa nyanya zilizopangwa vizuri. Haikuchukua hata dakika mbili nilipojigeuza, Brian alikuwa ametoweka. Panic ilinishika.

Nilimuita kwa sauti ya juu, nikakimbia huku na kule, nikawauliza watu waliokuwa karibu lakini hakuna aliyeona chochote. Masaa yaligeuka kuwa siku, siku zikawa wiki. Niliripoti polisi, wakachukua maelezo, wakaniambia nisubiri uchunguzi.

Nilizunguka kila kituo cha polisi, nikachapisha picha yake, nikatangaza hadi redioni, lakini kila siku iliisha bila jibu. Mume wangu alianza kunilaumu kwa uzembe. Familia ilianza kunitenga kana kwamba nilikuwa na mkono katika kupotea kwa mwanangu.

Hali ya ndoa ilianza kuyumba, na hata nilipojaribu kuwa na imani, ukweli ni kwamba nilianza kukubali kuwa huenda sitamwona tena Brian. Maisha yangu yalikuwa ya huzuni, machozi, na majuto. Hakukuwa na raha tena. Kila mtoto niliyemuona barabarani alinikumbusha mwanangu aliyepotea. SOMA ZAIDI.
Share To:

Post A Comment: